Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ramadhan Omary achaguliwa kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TMA
Habari Mchanganyiko

Ramadhan Omary achaguliwa kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TMA

Spread the love

 

WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wamemchagua, Ramadhani Omary kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa TMA, kupitia kikao cha Baraza hili kinachoendelea Morogoro tarehe 03 na 04 Aprili 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Omary alichaguliwa kwa kupata kura 62 akifuatiwa na Katibu Msaidizi, Mecklina Merchades kura 32, jumla ya kura zilizopigwa ni 94. Uchaguzi huo umesimamiwa na Christina Matega, Afisa kazi kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Morogoro.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo lilitambulisha wimbo wa TUGHE-Taifa na kuzindua rasmi kipeperushi maalumu na bango la TUGHE-TMA ambavyo vitatumika katika kuitangaza TUGHE-TMA kwenye majukwaa mbalimbali kupitia dhana ya uzalendo, ubunifu na uwajibakaji.

Omary ni Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka Ofisi ya Kituo Kikuu cha Utabiri, dawati la utabiri wa muda mrefu, anachukua nafasi ya Chuki Sangalugembe aliyemaliza muda wake kwa mujibu wa mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa TMA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!