Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango ataka mambo sita yazingatiwe uandaaji Dira ya Taifa 2050
Habari za Siasa

Dk. Mpango ataka mambo sita yazingatiwe uandaaji Dira ya Taifa 2050

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais, Dk. Phillip Mpango, ametaka mambo sita yazingatiwe katika uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mpango ameyataja masuala hayo leo tarehe 3 Aprili 2023, akizindua mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, jijini Dodoma.

Jambo la kwanza alilotaja Dk. Mpango, ni kuangalia namna ya dira hiyo itakavyoweza kuimarisha uwezo wa kiuchumi uliojengwa, pamoja na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

Dk. Mpango amesema jambo la pili linalopaswa kuzingatiwa ni kuangalia namna gani dira hiyo itatumia fursa ambazo hazijatumika ipasavyo, pamoja na kuzishikilia fursa zinazochipukia hususan katika kilimo kwa kuhakikisha mikakati inawekwa ili Tanzania iwe ghala la chakula barani Afrika na duniani.

“Kwanza katika kilimo Tanzania ina fursa kubwa kuwa ghala la chakula Afrika, mashariki ya kati na duniani, kama tukilenga uzalishaji mkubwa wa mahindi, ngano, shairi, maharage, soya, sukari, mafuta ya kupikia, korosho, matunda , mboga mboga na viungo,” amesema Dk. Mpango.

Katika eneo hilo, Dk. Mpango ameagiza dira hiyo izingatie matumizi ya rasilimali zinazotokana na mifugo na uvuvi, katika uwekezaji wa viwanda. Matumizi ya mazao ya misitu na namna ya kuongeza thamani mazao ghafi ya madini na gesi asilia.

“Eneo lingine tuangalie uvunaji rasilimali za kimkakati ili kujenga viwanda. Tuna gesi asilia na kwa hiyo tuna fursa ya kujenga kiwancha cha kuchakata gesi asilia. Pia, viwanda vya kemikali ikiwemo mbolea, tuna makaa ya mawe na chuma na nikeli ambayo tunaweza kutumia kujenga kiwanda cha betri,” amesema Dk. Mpango.

Dk. Mpango ameagiza dira hiyo izingatie namna ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji katika nchi za maziwa makuu.

“Tuna fursa ya kila aina, tuna fursa ya kutumia miji yetu inayokuwa haraka, uvunaji na matumizi ya nishati jadidifu ikiwemo joto ardhi, mawimbi ya bahari na upepo na matumizi ya taka ngumu kuzalisha mbolea na bio gesi,” amesema Dk. Mpango.

Makamu huyo wa Rais, ameagiza maandalizi ya dira hiyo, yazingatie namna ya matumizi ya nguvu kazi ya vijana iliyopo nchini katika kuimarisha uchumi, pamoja na kutangaza fursa ya lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Kitanzania.

Katika hatua nyingine, amezitaka taasisi na idara za Serikali na sekta binafsi, kutoa ushirikiano wao katika uwasilishaji mapendekezo yao ili yawekwe kwenye dira hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!