Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto atia neno maandalizi Dira ya Taifa 2050
Habari za Siasa

Zitto atia neno maandalizi Dira ya Taifa 2050

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameshauri mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uwe wa wazi pamoja na kushirikisha makundi mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia na vijana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto ametoa wito huo leo tarehe 3 Aprili 2023, muda mfupi baada ya Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango, kuzindua mchakato huo jijini Dodoma.

“Mchakato wa kuandika Dira ya Maendeleo, uwe wa wazi kwa kushirikisha CSOs vya kutosha, vijana wa sasa ndio wastaafu wa 2050, washiriki kuandaa ndoto ya Tanzania yao wanayotaka kustaafishwa. Kama kamati ya kuandaa Dira ina watu 20, basi vijana wawe 10 ( 5 vijana wa kike na 5 vijana wa kiume),” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Katika hatua nyingine, Zitto amealika Serikali kufanyia kazi dira ya ACT-Wazalendo, katika maandalizi ya dira hiyo.

Zitto ameshauri mikakati madhubuti iwekwe itakayowezesha Pato la Taifa kukua zaidi ya mara sita ilivyo sasa, hadi kufikia Dola za Marekani 455 bilioni.

“Inawezekana mwaka 2000 GDP yetu ilikuwa Dola 13 bilioni na sasa ni Dola 70 bilioni. Lakini kazi kubwa ya ku ‘transform’ uchumi inahitajika ikiambatana na nidhamu ya hali ya juu. Tutahitaji uchumi wetu ukue kwa kasi ya wastani wa 8% kwa mwaka kwa miaka 10 mfululizo ya mwanzo na kasi isipungue 6% kwa miaka mingine 10 hadi kufikia 2050,” ameandika Zitto na kuongeza:

“Miaka 10 ya mwanzo kilimo kinapaswa kuwa sekta kuu ya kuchochea ukuaji wa uchumi ambapo kasi yake ya kukua isiwe chini ya wastani wa 6-8% kwa miaka hiyo 10 mfululizo. Kilimo kikikua kwa 10% kama shabaha ya ajenda 2030 ilivyo, uchumi utafurumia! Itakuwa achievement kubwa mno.”

1 Comment

  • (i) Ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto kwa misingi ya makabila, lugha na dini umeenea duniani na kuleta athari kwenye mfumo wa haki, usawa na hata KUJISOMEA, limesema Shirika la UN la UNICEF.
    (ii) South Sudan’s refugee crisis remains the largest in Africa. Those displaced within and from South Sudan jointly call for an end to the /conflict for a chance to return to a peaceful home.
    (iii) UNHCR’s support for ~1 million Rohingya refugees in Bangladesh is underfunded. Critical services such as health, housing, water, sanitation and hygiene are at risk.
    (iv) On average, over 40 million people have been estimated to be food insecure every year by the SADC Regional Vulnerability Assessment Programme over the past five years.
    (v) Balaaa NA NI HATARI: Wagandana wakifanya mapenzi, aliewanasisha aeleza alivyofanya, mganga atoa masharti mazito.
    (vi) Wamiliki wa ardhi katika kata ya Mabwepande Wilaya ya Kindondoni jijini Dar es Salaam wameililia serikali wakitaka kuondolewa kwa wavamizi wa ardhi eneo hilo wanaodaiwa kuhatarisha usalama.
    (vii) Americans watched in horror as the terrorist attacks of Sept. 11, 2001, left nearly 3,000 people dead in New York City, Washington, D.C., and Shanksville, Pennsylvania.
    (viii) Mwalimu alikuwa anafundisha shule ya vichaa na alijiwekea utaratibu kuwa kila mwisho wa mwaka atawapa jaribio nani amejaribu kupona ukichaa siku moja alipokuwa darasani alichora mlango ubaoni.
    (ix) Utafiti mkubwa uliofanywa duniani na kuchapishwa katika jarida la lancet umethibitisha kwamba utafiti uliofanywa awali na kuonyesha kwamba hakuna usalama katika unywaji wa pombe.
    (x) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 hayakuwa ya bahati mbaya wala yasiyoweza kuepukika.
    (xi) Mhe. WAZIRI Mkuu baada ya SERIKALI KUHAMIA DODOMA LINI VYOMBO VYA HABARI VYA ITV, EATV, TBC, AZAM TV, WASAFI TV, MWANANCHI VITAHAMIA DODOMA KWA LAZIMA.(TULIBUNI DSM HATUWEZI KUBUNI DODOMA)SWAHILI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!