Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais wa Romania awasili rasmi nchini
Habari za Siasa

Rais wa Romania awasili rasmi nchini

Spread the love

Rais wa Romania, Klaus Iohannis, amewasili nchini kwa ziara ya kitaifa kuanzia leo tarehe 16 hadi 19 Novemba 2023 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki.

Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kushawishi uwekezaji zaidi na kuvutia watalii wengi kutoka nchini Romania.

Aidha, katika mazungumzo rasmi yatakayofanyika tarehe 17 Novemba 2023 Rais huyo na mwenyeji wake watajadili namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati sekta za elimu, afya, kilimo nishati na madini.

Kabla ya kuondoka nchini tarehe 19 Novemba 2023, Rais wa Romania atapata fursa ya kwenda Zanzibar ambapo atazungumza na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi na kutembelea mji mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii duniani

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!