Wednesday , 22 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Kagera aonya madai chanzo vifo watoto sita kuwa kuku wa wizi
Habari MchanganyikoTangulizi

RC Kagera aonya madai chanzo vifo watoto sita kuwa kuku wa wizi

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa amewaonya wananchi wa Kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo na wilaya jirani kuacha kusambaza taarifa za uongo kuwa watoto sita wa familia moja waliofariki kwa nyakati tofauti kwamba walikula kuku wa wizi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amewataka wananchi hao kupuuza taarifa hizo kwa kuwa ni minong’ono iliyoenea katika kijiji hicho na hata nje ya mkoa huo wa Kagera hali inayozua taharuki bila kuwepo na ushahidi wa kutosha.

Akizungumza katika mazishi ya watoto hao wa familia ya Lazaro Sanabanka yaliyofanyika jana, Mwasa alisema ameunda tume ili kuchunguzi tukio hilo hasa ikizingatiwa chanzo kinasadikiwa kuwa walikuwa mboga za majani aina ya maharage ya kunde yanayodaiwa kuwa na sumu.

“Tusitilie maanani ‘rumors’ hizo, tunaendelea na uchunguzi wa kina na kupima sampuli zao ikiwamo mboga za majani shambani.

“Lengo ni kupata uthibitisho kuona uhakika ni sumu ya aina gani, haya ya kutuhumiana tuachane nayo maana wengine wameanza kusema unajua kuku wa jirani aliibiwa… Tusiende huko! Kama tuna imani ya dini zetu, tufuate maelezo ya mkuu wa wilaya,” alisema.

Mbali na kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa familia hiyo, Mkuu huyo wa mkoa alisema wamegharamia mazishi hayo kwa kuchonga majeneza, chakula cha maomboleza na kutoa ubani ambao hakutaja kiasi chake

Akisimulia mkasa ulioikumba familia yake, Lazaro Sanabanka alisema wakiwa shambani pamoja na mkewe walipokuwa wanaandaa shamba kwa ajili ya kupanda mahindi walipata taarifa kuwa mtoto wao mmoja anaumwa.

Alisema mama aliporudi alikuta mtoto huyo anadhoofu mithili ya mtu mwenye degedege na hata alipopelekwa hospitali hali ilikuwa mbaya na huku nyumba kwa nyakati tofauti watoto wengine walianza kuumwa.

Alisema watoto hao waliwaeleza kuwa walimchinja kuku wa jirani ambao aliingia ndani kwao.

Alisema asubuhi ya siku iliyofuata mtoto mwingine alianza kuumwa na kufuata watoto wengine ambao licha ya kuwakimbiza hospitali watano walifariki dunia.

Baba huyo wa familia, alisema hana ugomvi na watu na hata jirani aliyedaiwa kuwa kuku alikuwa wa kwake, walipoenda nyumbani kwake hawakumkuta.

Baadhi ya majirani waliozungumza na waandishi wa habari, akiwamo Emanuel Gervas Kapela alisema wanalaani tukio hilo ili lisijirudie tena katika kijiji hicho.

Hata hivyo, alisema taarifa za kuwa chanzo cha vifo hivyo ni kuku wa wizi, hizo ni imani kwa kuwa kuku huyo aliliwa siku nyingi.

Aliongeza kuwa chakula cha usiku kilichodaiwa kuwa na mboga zenye sumu, ni majani yan maharage licha ya kwamba sio wote wa familia hiyo waliopata matatizo hayo.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa vimetokea kwa nyakati tofauti baada ya wanafamilia 11 kula chakula cha usiku tarehe 13 Novemba 2023.

Chatanda alisema wanafamilia hao baada ya kula chakula cha usiku walienda kupumzika  lakini asubuhi yake watoto watatu  Brayan Ezekiel (2), Kahindi Samson (9) ambaye ni mwanafunzi wa awali shule ya msingi Muungano na Happines Razaro (12) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Muungano walianza kujisikia vibaya wakakimbizwa kituo cha afya Nyakanazi wakati wanaendelea na matibabu tarehe 14 Novemba 2023 wakapoteza maisha.

Alisema watoto wengine watatu walianza kujisikia vibaya nao walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya wilaya ya Biharamlo wakati wakiendelea na matibabu tarehe 15 Novemba 2023 wawili walipoteza maisha na hivyo idadi ya waliofariki kuwa watano

Wawili waliofariki ni Melisiana Razaro (11) na Melina Razaro (9) huku Josephina Juma (5) aliyekuwa akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo naye jana tarehe 16 Novemba amedaiwa kufariki dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

error: Content is protected !!