Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Wanasiasa tusiburuze wananchi mchakato wa katiba mpya
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Wanasiasa tusiburuze wananchi mchakato wa katiba mpya

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amevitaka vyama vya siasa kutohodhi mchakato wa marekebisho ya katiba, akisema suala hilo si mali yao bali ni mali ya wananchi wote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akifungua mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa, leo tarehe 11 Septemba 2023, jijini Dar es Salaam, Rais Samia amewataka wanasiasa kutowaburuza wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba.

Mkuu huyo wa nchi, amesema mchakato huo utaanza na utoaji elimu kwa wananchi ili waielewe katiba, kwa kuwa asilimia kubwa hasa walioko vijijini hawaijui vyema.

“Tunaanza na elimu ya katiba, watanzania wajue ni kitu gani, wajue kinasemaje na kina nini sababu tunakokwenda viongozi wa kisiasa tunadhani tuna haki ya kuburuza watu.

Tunachokisema sisi watu wote wafanye hivyo. Katiba si kitabu ni morality ethical standard, tutaenda kwa mwendo huu kila mtu ajue,”amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “tuna kazi kubwa ya kuwafanya watanzania waijue katiba ni nini na hiko kitabu kimekaaje. Wengine hawakijui ukienda huko vijijini mtu anaweza akaja na Ilani ya CCM akakwambia katiba, hajui ilani inasemaje wala katiba inasemaje hawajui.”

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema kamati maalumu itaanzishwa kwa ajili ya kusimamia mchakato huo, ambapo vyama vya siasa vitatoa uwakilishi wake.

“Tusiwaburuze, katiba viongozi wa siasa si yetu ni mali ya watanzania. Mwisho wa mkutano huu nimemwambia msajili nataka viongozi wa vyama walete maoni yao kwenye kamati itakayokwenda kuanzisha mchakato wa katiba na ninyi mtakuwa na wawakilishi wenu sio kila mtu ataingia kule,” amesema Rais Samia.

Msimamo wa Rais Samia kuanza kutoa elimu kwa wananchi juu ya katiba, umepinga vikali na baadhi ya makundi ikiwemo asasi za kiraia, ambayo yameshauri mchakato huo uanze moja kwa moja katika marekebisho kwa madai kuwa elimu ilishatolewa hapo awali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!