Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia airushia dongo Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia airushia dongo Chadema

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema kuna chama kikipewa madaraka baadhi ya viongozi wake wataunda chama kingine ili wawapinge wenzao walioko madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa, leo tarehe 11 Septemba 2023, jijini Dar es Salaam, akizungumzia baadhi ya vyama vinavyodaiwa kutumia vibaya uhuru wa kutoa maoni kwa kutoa lugha za uchochezi.


“Mwingine kaumbwa hivyo roho yake basi tu, raha yake aone ugomvi na mabishano  na huyo amua leo mwambie mimi nakupa Serikali na wenzio kikundi, ataunda chama kingine awapinge wale wenzio aliokuwa nao,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amedai baadhi ya vyama vya siasa vinavyosusa kushiriki mikutano ya kitaifa inayoitishwa kwa ajili ya kutafuta maridhiano, ndani yake hakukaliki.

“Na ndiyo tunayoyaona huko kwao, ukiona hawapo hapa sio tu labda kuna kununa huko hakukaliki. Humo ndani kuna moto wengine twende wengine tusiende. Kwa tabia kama zile watakuwa na amani kweli? Hawawezi kuwa na amani kwa hiyo ndugu zangu uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake,” amesema Rais Samia.

Bila ya kutaja jina, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekuwa kinara wa kususia mikutano ya kitaifa inayoandaliwa kwa ajili ya kujadili hali ya kisiasa nchini ambapo Rais Samia alisema baada ya kususa kushiriki katika kikosi kazi alichokiunda kuangalia namna ya kuboresha demokrasia ya vyama vingi, aliamua kukisikiliza peke yake kwa ajili ya kupata mapendekezo yake.

Baada ya Chadema kususia mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika Desemba 2021 na kugoma kushiriki katika kikosi kazi hicho, Rais Samia aliunda kamati maalum ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Bara, Abdulrahman Kinana, iliyoketi na  wajumbe wa chama hicho cha upinzani , kwa ajili ya kusikiliza mapendekezo yao.

“katika kuleta wote twende pamoja nilichukua njia nyingine ya kukaa na chama kingine ambacho kilikuwa hakitaki kuingia kwenye ule mfumo wa kikosi kazi na Baraza la Vyama vya Siasa, nikasema ngoja niwasikilize , nikatoa fursa ya kuwasikiliza na mapendekezo yao hayana tofauti na yaliyotolewa na vikosi kazi viwili,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewataka wanasiasa kufuata sheria ili kudumisha amani na umoja wa kitaifa.

Kuhusu mikutano ya hadhara, Rais Samia amevitaka vyama vya siasa kutoitumia fursa hiyo kutoa kauli za kuwagawa wananchi bali viitumie kutangaza hoja na sera zake kwa ajili ya kutafuta uungwaji mkono katika chaguzi.

“Tumeruhusu mikutano tukiwa na nia vyama vizungumze wananchi wasikie sera , mada na mipango yao ili vikue na virudishe waliowapoteza visimame madhubuti tukienda kwenye chaguzi, hatukutoa ruhusa ili watu wavunje sheria, wakasimame kutokana, kukashifu na kuchambua dini za watu,” amesema Rais Samia.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, changamoto ya baadhi ya vyama vya siasa kutoa lugha za matusi katika mikutano ya hadhara, inatokana na kukosa ajenda za kuzungumza.

“Lakini si shangai kwa nini haya yanatokea sababu yakuzungumzwa hakuna, tulianza na katiba, tukaenda ikakatika katikati. Bandari imeenda sasa katiba tena hakuna, kwa hiyo unapokuwa hakuna unalazimisha ufanye jambo utazungumza na yasiyokuwepo au yasiyo katika muelekeo huo,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!