IDADI vifo katika tetemeko la ardhi lilitokea usiku wa tarehe 8 Septemba 2023 katika miji kadhaa nchini Morocco, vimeongezeka kutoka 2,122 hadi 2,500. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa.
Idadi hiyo imetajwa kuwa inazidi kuongezeka kutokana na ukubwa wa tetemeko hilo ambalo limeharibu majengo na makazi ya watu, wengi wao wakiwa wamepoteza maisha kwa kufukiwa na vifusi huku wengine wakipota kusikojulikana.
Aidha, mmoja wahanga wa tetemeko hilo aliyejitambilisha Hassan ni mmoja wa wahanga wa tetemeko katika kijiji hicho kilichopo nchini humo, amesema ameweza kujiokoa kutoka kwenye kifusi hicho lakini mjomba wake bado amezikwa chini ya vifusi na hakuna nafasi kwamba anaweza kuwa hai.
“Hakukuwa na wakati wa kutoka na kujiokoa,” amesisitiza Hassan.
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani wa nchi hiyo imesema; “Watu wengine 2,476 walijeruhiwa ambayo kutokana na tetemeko hilo.”
Leave a comment