Thursday , 13 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba amkumbusha Samia Katiba mpya kwa maandalizi uchaguzi 2024, 2025
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba amkumbusha Samia Katiba mpya kwa maandalizi uchaguzi 2024, 2025

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibahimu Lipumba amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza ahadi yake ya kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa kuwa itajenga mazingira mazuri ya kisiasa na kumfanya kuwa na ajenda nzuri kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

Ptof. Lipumba ameyasema hayo leo tarehe 11 Septemba 2025 wakati akihutubia Mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa unaofanyika Jijini Dar es salaam uliofunguliwa Rais Samia ambaye pia alikuwa mgeni rasmi.

Profesa Lipumba ameeleza kuwa TCD ilifanya mkutano na wadau wa kitaifa kujadili hali ya kidemokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 ambapo kwenye mkutano huo kuna mambo kadhaa yaliazimiwa ikiwa ni pamoja kuendelea kwa mchakato wa kupatikana katiba mpya.

Pia Lipumba amesema kuwa baada ya kubaini muda huenda usitoshe kupatikana kwa katiba mpya kwa wakati, wanapendekeza yatumike mapendekezo yaliyotolewa na TCD wakati wa uongozi wa Abdulrahman Kinana kutaka kufanya marekebisho madogo madogo ili kujenga mazingira mazuri kuelekea chaguzi hizo.

“Tumezungumzia suala zima la tume huru ya uchaguzi na hususani kufanya mabadiliko ya ibara ya 74 ya katiba ya sasa, tume huru hiyo isimamia uchaguzi mkuu na vilevile uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Kuwepo kwa mgombea binafsi, kufanya marekebisho ibara ya 39(2) ya katiba ya sasa kuhusu Rais na ibara ya 67 kuhusu wagombea ubunge. Kuwa Rais atangazwe akishinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote kwa hiyo kurekebisha ibara ya 41 (6) na vilevile uchaguzi wa Rais uweze kuhojiwa mahakamani kwa kubadilisha ibara ya 41 (7),” amesema na kuongeza;

“Na nina imania ikiwa mambo haya utayasimamia pia inaweza ikawa agenda nzuri ya kwako kwamba nahitaji kukamilisha mabadiliko niliyoyaanzisha na ukienda na agenda hiyo 2025 patakuwa na kazi kubwa ya kuweza kuipiku ajenda hiyo,” ameongeza Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba pia amempongeza Rais Samia kwa kukipa uhai wa kujiendesha na kutekeleza majukumu yake kituo hicho cha demokrasia Tanzania tangu alipoingia madarakani mwaka 2021.

Vile vile Profesa Lipumba amempongeza Rais kufungulia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

“Rais umefungua mikutano ya hadhara, na nitakwenda Tabora na nitafanya mkutano wa hadhara hapa sihitaji kubadilisha hii kuwa mkutano wa hadhara nakushukuru sana. Asante sana,” amemalizia Lipumba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

error: Content is protected !!