Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Tunakamilisha mchakato Chato iwe mkoa
Habari za Siasa

Rais Samia: Tunakamilisha mchakato Chato iwe mkoa

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali anayoingoza inakamilisha mchakato wa kuifanya Chato kuwa Mkoa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 14 Oktoba 2021, katika Uwanja wa Magufuli, Chato mkoani Geita katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya kifo cha miaka 22 ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Pamoja na kuwaombea, Marais wastaafu, Benjamin Willium Mkapa na John Pombe Magufuli.

Rais Samia amesema, katika kumuenzi Hayati Magufuli aliyefariki dunia 17 Machi 2021, akiwa madarakani, walimua shughuli hizo kitaifa, zifanyikie wilaya ya Chato, sehemu aliyozaliwa Hayati Magufuli.

“Tumesukumwa na uamuzi wa kuja Chato ili kumuenzi mpendwa wetu Hayati Magufuli ambaye ni mzaliwa wa Chato, aliyepapenda sana nasi tunaendeleza upendo wake. Ili kumuenzi tumeamua kuja kufanya sherehe hizi ambazo kwa kawaida hufanyika makao makuu ya mkoa,” amesema Rais Samia huku akishangiliwa.

Ametumia fursa hiyo kuwaeleza kuwa “yapo mambo ambayo Hayati Magufuli aliwaahidi wana Chato wakati wa kampeni. Mambo hayo ni upanuzi wa Bandari ya Nyamilembe, kumamilisha Uwanja wa Ndege wa Chato, Hospitali ya Kanda ya Chato, Chuo cha Veta na mimi niwaahidi yote yatatekelezwa.”

Huku shangwe zikitawala uwanjani hapo, Rais Samia akasema, lipo jambo ambalo wananchi wa Chato wangependa kulisikia kutoka kwake. Kauli hiyo ilizidisha shangwe zaidi na yeye akasema “Serikali inakamilisha vigezo vinavyoruhusu Chato kuwa Mkoa. Kuna vigezo kadhaa ambavyo bado tunaendelea kuviangalia na vigezo hivi vikikidhi tunakwenda kulimaliza jambo hili.”

Mchakato wa Chato kuwa Mkoa, ulianza enzi za utawala wa Hayati Magufuli na wakati wa maziko yake, tarehe 26 Machi 2021, wazee wa Chato walimwomba Rais Samia aliyeingia madarakani baada ya kifo hicho cha Magufuli, kuendeleza ndoto hiyo na kuufanya Chato kuwa mkoa.

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge wa Uhuru

Rais Samia aliagiza mchakato kuanza na mara utakapokamilika, wataangalia jinsi ya kufanya.

Tayari vikao kadhaa vimefanyika katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma na Geita vimekwisha kufanyika kwa nyakati tofauti ili kuruhusu baadhi ya wilaya zake kugemwa ili kuunda mkoa huo mpya wa Chato.

Baadhi ya Wilaya zinazotarajia kuunda Mkoa wa Chato ni Chato yenyewe, Ngara, Biharamulo, Bukombe huku Kata tatu za Wilaya ya Muleba zikihamia Chato huku Hifadhi ya Taifa ya Rubondo itakuwa Chato.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!