October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Miradi 49 yenye dosari, Rais Samia atoa maagizo

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge wa Uhuru

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameagiza mamlaka zifanye uchunguzi taarifa ya ya miradi 49 iliyobainika kuwa na dosari katika Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru mwaka 2021, ili wahusika wachukuliwe hatua. Anaripoti Reginba Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo, leo Alhamisi, tarehe 14 Oktoba 2021, katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, kilichofanyika Uwanja wa Magufuli, wilayani Chato, Mkoa wa Geita.

Ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) pamoja na wizara zinazosimamia sekta za miradi hiyo, zifanyie kazi taarifa iliyotolewa na kiongozi wa mwenge huo, Luteni Josephine Mwambashi.

Ni baada ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge , Ajira Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, kubainusha miradi hiyo yenye thamani ya Sh.65.3 bilioni kubainika kuwa na dosari hivyo kutofunguliwa.

“Tumesikia Jenista na kiongozi wa mwenge wametupa taarifa kuhusu miradi 49 yenye hasara ya Sh. 65.3 bilioni, haijazinduliwa na mwenge wa uhuru kwa sababu ya dosari mbalimbali ikiwemo yenye viashiria vya ubadhirifu na iliyotekelezwa chini ya viwango,” amesema.

“Utakuta rushwa ni moja ya sababu ya miradi kutotekelezwa kwa ufanisi. Matumaini yangu ofisi ya waziri mkuu, Takukuru na wizara zinazosimamia sekta husika, zitaifanyia kazi taarifa hiyo na kuchukua hatua muafaka bila kumuonea mtu muhali,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza akisema “na kwa wale wote watakaobainika kuathiri utekelezaji miradi hiyo kutokana na uzembe na rushwa, hatua stahiki zichukuliwe.”

Wakati huo huo, Rais Samia amehoji kwa nini wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yao wanashindwa kubaini dosari zinazojitokeza katika miradi yao.

“Hapa kuna swali najiuliza kwa nini viongozi wa maeneo hayo, wakuu w a mikoa, wilaya, wakurugenzi na maafisa Takukuru wanasubiri mpaka wakati wa mbio za mwenge unapita kujua dosari za miradi hiyo, kwa nini kuna hilo tatizo?,” amesema Rais Samia.

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge , Ajira Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama

Rais Samia ameonya kuwachukulia hatua viongozi wa mikoa ambayo dosari hizo zitajitokeza.

“Miradi hii inajengwa kwenye maeneo ambayo viongozi wapo, mkuu wa mkoa, wakuu wa wilayani, wakurugenzi na maofisa wa Takukuru wapo ila wanasubiri hadi mwenge wa uhuru.”

“…kwa nini yanatoeka bila kuchukua hatua? Hii sababu hakuna ufuatiliaji wakati miradi hii inatekelzwa, naomba nitoe midhari miradi inayotekelezwa dosari hizi zisijitokeze na kama nilivyosema juzi nitasimama imara kufuatilia utekelezaji miradi ile lakini miradi mingine,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Niwatake viongozi wa maeneo ninapozima mwenge mwakani idadi ya dosari ipungue sana na kwa ile miradi au mikoa bado itajitokeza ina miradi yenye dosari, tutaelewana wakati huo, hii ni onyo kwa wakuu wa mikoa na wilaya, lakini wakurugenzi wa halmashauri pia.”

error: Content is protected !!