Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwenge wa Uhuru waziweka wilaya 38 kikaangoni
Habari za Siasa

Mwenge wa Uhuru waziweka wilaya 38 kikaangoni

Spread the love

 

ZEGE halilali, ndivyo unavyoweza kutafsiri kilichoibuliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu ambapo jumla ya miradi 49 yenye thamani ya Sh bilioni 65.3 imebainika kuwa na dosari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Hilo limethibitishwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka huu, Luteni Josephine Mwambashi baada ya kusoma risala ya wakimbiza mwenge kutoka JWTZ na kumkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan taarifa ya kina kuhusu dosari hizo pamoja na uchunguzi wa awali wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

Akisoma risala hiyo leo tarehe 14 Oktoba, 2021 katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru mkoani Geita ambacho kimefanyika sambamba na maadhimisho ya kumbukizi ya kifo cha Mwalimu Nyerere pamoja na wiki ya vijana, Luteni Josephine amemuomba Rais Samia kuunda kamati maalumu kuchunguza dosari hizo.

Amesema katika mbio hizo za Mwenge zilizozinduliwa Mei 17 mwaka huu mkoa wa Kusini Unguja huko Visiwani Zanzibar umekimbiziwa kwa siku 150 katika mikoa 31.

“Mwenge wa Uhuru umekagua miradi 1060 yenye thamani ya Sh trilioni 1.2, miradi iligusa sekta za kipaumbele kama vile afya, maji, elimu, barabara na kilimo,” amesema.

Amesema lengo la Mwenge huo wa uhuru ni pamoja na kuhamasisha, amani, umoja, upendo na maendeleo.

“Ajenda kubwa ya Mwenge wa Uhuru ilikuwa matumizi sahihi ya Tehama. Mwenge umefanya kazi wa kutathmini na kuhimizia matumizi ya Tehama katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kwenye halmashauri zetu.

“Hata hivyo, tumebaini bado kuna vyanzo havijaingizwa kwenye mifumo ya kielektroniki, hivyo tumewahimiza viongozi waliopewa dhamana kuhakikisha kwamba vyanzo vyote vinaingizwa kwenye nmifumo ya Tehama ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.

“Lakini tumetoa tahadhari kuhusu matumizi mabaya ya Tehama kwani inaweza kuhatarisha usalama wa taifa, kupitia mitandao ya kijamii na matumizi mabaya ya Tehama kwa ujumla,” amesema.

Aidha, alitaja baadhi ya kasoro katika miradi hiyo 49 kuwa ni pamoja na miradi kujengwa kinyume na makubaliano na mikataba na kutozingatia taratibu za fedha za umma.

“Kutoheshimu na kutotumia kamati za ujenzi za wilaya, kutotumia wakandarasi kwa kina, upotevu na ufichaji wa nyaraka za malipo, matumizi mabaya ya fedha za umma, udanganyifu kwa kutumia lugha za kitaalamu na wakandarasi kulipwa fedha hewa.

“Nyingine ni kutowashirikisha wananchi wakati wa kupanga na kutekeleza miradi. Kuweka gharama kubwa zisizoendana na bei, vitendo hivi vinahujumisha taifa na kuenda kinyume na force akaunti,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!