Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Rais Samia: Magari ya wagonjwa 213 mabovu, halmashauri 33 zaathirika
Afya

Rais Samia: Magari ya wagonjwa 213 mabovu, halmashauri 33 zaathirika

Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema magari ya kubebea wagonjwa 213 kati ya 444 ni mabovu, huku halmashauri 33 zikiwa hazina hata moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo tarehe 28 Oktoba 2023, akizungumzia ujio wa magari 989 ambayo yemeagizwa na Serikali, kwenye hafla ya uzinduzi wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria kwa 2022.

“Hali ilivyo sasa tuna magari 444 ambayo 213 ni mabovu kabisa na halmashauri 33 hazina gari hata moja la wagonjwa. Sasa mgawo huu wa leo na magari yanayokuja kila halmashauriitapata gari la wagonjwa,” amesesema Rais Samia.

Rais Samia amesema hadi sasa Serikali imegawa magari 216, kati ya 989 yaliyonunuliwa.

“Mengi yamefanywa na Serikali yalikwisha elezwa na mawaziri, leo tumegawa magari 216 ya kubeba wagonjwa na 153 kwa ajili ya usimamizi, uratibu wa shughuli za afya na utoaji huduma za mkoba katika halmashauri zetu. Hapa nataka niseme magari tuliyogawa leo ni kati ya magari 989 ambapo 369 tumeshayapokea,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema Serikali imegawa seti 123 za vifaa vya huduma kwa watoto wachanga na wenye uzito pungufu, ili kupunguza vifo vya watoto njiti. Mashine 125 za mionzi na mashine 140 za kutibu saratani ya mlango wa kizazi kwa kina mama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!