May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia kuteta na wanawake Dodoma kesho

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumanne, tarehe 8 Juni 2021, kuanzia saa 3:00 asubuhi, atazungumza na wanawake wa mkoa wa Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ni katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convertion Center, uliopo jijini Dodoma.

Akizungumzia mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema, Rais Samia atazungumza na wanawake zaidi ya 10,000 wakiwakilisha wanawake wote nchini.

Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Mtaka amesema, wanawake wa Wilaya ya Dodoma na maeneo jirani, wamekwisha kupewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo pamoja na wabunge wanawake bila kujali vyama vyao wamealikwa kushiriki.

Hii itakuwa mara ya pili, Rais Samia kukutana na kuzungumza na makundi maalum, ikitanguliwa na mazungumzo aliyoyafanya na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.

error: Content is protected !!