Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Bocco, Dube hapatoshi
MichezoTangulizi

Bocco, Dube hapatoshi

Prince Dube
Spread the love

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara inaelekea ukingoni huku kukiwa na vita tatu tofauti katika maeneo mablimabli kwenye msimu huu wa 2020/21, huku vita inayoangaliwa kwa sasa ni vita ya upachikaji mabao kati ya John Bocco mshambuliaji wa Simba pamoja na Prince Dube kutoka Azam Fc. Anaripoti Mwandishi Wetu

Wawili hao wameingia kwenye vita ya kunyakuwa kiatu cha mfungaji bora mara baada ya kupishana kwa bao moja katika msimamo wao.

Prince Dube kutoka Azam FC yupo kileleni akiwa na jumla ya mabao 14 aliyocheza akiwa na Azam FC toka alijiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu wa 2020/21.

Nafasi ya pili inashikiliwa na John Bocco ambaye amekuwa na moto mkali toka aliporudi kutoka kwenye majeraha nakufikisha jumla ya mabao 13.

John Bocco mshambuliaji wa Simba

Wawili hao walikuwa kwenye majeruhi katika kipindi tofauti lakini walirejea wakiwa na makali yao ya kufumania nyavu katika michezo ya Ligi Kuu.

Katika michezo yake mine toka aliporejea kutoka kwenye majeruhi John Bocco amepachika jumla ya mabao saba na kuwa mshambuliaji kinara wa mabao ndani ya klabu ya Simba na kupachika mabao Zaidi ya 12 katika kipindi cha misimu saba.

Ukiachia Ligi Dube mpaka sasa amepachika jumla ya mabao 17 katika michezo 27 aliyoichezea Azam Fc katika michuano tofauti kiasi cha kuwavutia matajiri wa timu hiyo kumpa mkataba mpya utakaomfanya aendelee kusalia hadi 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!