Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Biashara Rais Samia azindua tawi la 230 NMB Kizimkazi Zanzibar
Biashara

Rais Samia azindua tawi la 230 NMB Kizimkazi Zanzibar

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan jana Jumatano amezindua Tawi la Benki ya NMB Paje, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar, uzinduzi unaoendelea kupanua mtandao wa matawi ya benki hiyo nchini na kufikia 230, yanayohudumia zaidi ya wateja milioni sita. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Uzinduzi huo ambao ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023), ulioweka rekodi ya mahudhurio makubwa ya viongozi waandamizi wa Serikali na wastaafu, umekuja siku 58 tangu Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango alipozindua tawi la 229 la Benki ya NMB Buhigwe mkoani Kigoma.

Rekodi ya mahudhurio makubwa ya viongozi waandamizi wa Serikali imewekwa katika uzinduzi wa NMB Paje, ambako ukiondoa Rais Samia, wengine waliohudhuria ni pamoja Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mizengo Pinda, pamoja na Mawaziri wa Wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Akitoa maelezo kwa Rais Samia, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,  Ruth Zaipuna alisema tawi hilo linaenda kumaliza changamoto ya wakazi wa Paje kusafiri umbali wa kilomita 60 kufuata huduma zetu za kibenki kwenye Tawi la Mwanakwerekwe.

“Karibu kutuzindulia Tawi la NMB Paje, ambalo ni la nne hapa visiwazi Zanzibar, lakini likiwa ni la 230 kwa mtandao mzima wa matawi yetu nchini Tanzania.

“Tuna imani kwamba tawi hili linaenda kuwasaidia sana wakazi wa mahali hapa, ambao awali walikuwa wanasafiri umbali mrefu wa takribani kilomita 60 kwenda Mwanakwerekwe kufuata huduma zetu za kibenki katika tawi letu kule.

“Tawi hili litatoa huduma zote za kifedha ikiwamo kufungua akaunti, kufanya malipo, kuweka ama kutoa fedha, huduma za bima, mikopo, pamoja na kubadili fedha za kigeni.

“Pia, wafanyakazi wetu wa tawi hili watatumia jengo hili kutoa Elimu ya Fedha kwa wananchi hasa wavuvi, wakulima wa mwani na wazalishaji chumvi, elimu ambayo tayari imeshaanza kutolewa hapa kabla hata ya uzinduzi huu unaofanyika leo,” alisema Zaipuna.

NMB Paje linakuwa ni tawi la 133 katika kipindi cha karibu miaka 26 ya benki hiyo ambayo ilikuwa na matawi 97 wakati ikianzishwa mwaka 1997.

NMB Tawi la Paje linakuwa ni la tatu kufunguliwa na benki hiyo mwaka huu 2023, likitanguliwa na matawi ya Kwa Mrombo jijini Arusha tarehe 3 Mei mwaka huu na Buhigwe Kigoma tarehe 4 Julai 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Mwezi wa kutoboa ni huu, cheza Keno Bonanza utusue Maisha

Spread the love MWEZI wa Oktoba wengi hupenda kuuita mwezi wakutoboa wakiwa...

Biashara

Wataalam Uganda wapewa darasa teknolojia mpya uchimbaji madini katika maonesho Geita

Spread the loveMAONESHO ya Teknolojia ya Madini yamezidi kuwa darasa kwa wadau...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!