Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina aibana Serikali kuadimika kwa dola
Habari za Siasa

Mpina aibana Serikali kuadimika kwa dola

Luhaga Mpina
Spread the love

MBUNGE wa Kisesa, ameihoji Serikali sababu za Dola za Marekani kuadimika nchini, wakati ikijinasibu kwamba kuna ongezeko la uwekezaji, utalii na mauzo ya nje. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mpina amehoji hayo leo tarehe 31 Agosti 2023, bungeni jijini Dodoma, akichangia hoja ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji, ya Bunge kuridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya 2012.

Alihoji hayo wakati akieleza umuhimu wa uwepo wa Dola za Marekani za kutosha, wakati Tanzania ikiridhia itifaki hiyo yenye lengo la kukuza ushirikiano wa nchi wanachama wa SADC katika biashara na sekta mbalimbali.

“Tunazungumzia ushirikiano wa sekta ya fedha nchini, hata SADC tunategemea dola na hamna zimeadimika. Wafanyabiashara hawapati dola hawawezi kuagiza mizigo sasa tunafanyaje? Maelezo yanayotolewa na Serikali ni kwamba utalii umeongezeka, uwekezaji umeongezeka maradufu sasa dola zimeenda wapi?” amehoji Mpina na kuongeza:

“Serikali lazima itatue tatizo la kuadimika kwa dola na hasa mimi ninavyoona sababu ziko nyingi zilizopelekea dola kuadimika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!