Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Othman: Tutumie rasilimali zetu kwa manufaa ya wote
Habari za Siasa

Othman: Tutumie rasilimali zetu kwa manufaa ya wote

Spread the love

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman yeye pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wako tayari kushirikiana na wawekezaji, Serikali zote na wadau wote ili rasilimali zilizopo zitumike kwa manufaa ya watu wote. Anaripoti Isaya Temu …(endelea).

Othman ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Agosti 2023 wakati akitoa salamu za Serikali ya ya Mapinduzi Zanzibar kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kufunga Tamasha la Kizimkazi ambalo limefanyika kwa sikua tano mfululio kwenye viwanja vya Paje, Mkoa wa Kusini Visiwani Zanzibar.

Pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote katika kuenzi hili tamasha hilo na kuhakikisha vivutio na rasilimali zinazopatikana katika Mkoa huo na Zanzibar kwa ujumla zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote.

Makamu huyo amesema licha ya mkoa huo kuwa mkubwa Visiwani Zanzibar ukiwa na kilomita za mraba 811, una idadi ndogo ya watu lakini pia ndio mkoa wenye vivutio vingi ikiwemo eneo la Makumbusho la Kizimkazi.

Pia amesema mkoa huo una Msitu wa Juzani ambao umepewa hadhi ya Kimataifa ya “biosphere reserve” ambazo kwa Tanzania ziko tano.

Amesema kuwa pamoja na kuwa na vivutio vyote hivyo bado hali ya maisha ya watu katika maeneo hayobado ni duni.

“Tunajiuliza kama tuna vivutio vyote hivyo, lakini bado tuna njaa” alisema Othman.

Hata hivyo, Makamu huyo amesema kuwa Rais Samia ameonyesha kuwa viongozi wanaweza kutenda vizuri zaidi kutumia rasilimali hizo kufaidisha watu.

“Leo umekuja kutuonesha ni namna gani tunaweza kutumia rasilimali hizi na tukashiba tukaenda upweo,” aliongeza Othman.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!