December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awageuzia kibao watumishi wa umma

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu, amewaagiza viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri, kutowafumbia macho watumishi wa umma wanaojihusisha na vitendo vya wizi, uzembe na upotevu wa fedha kazini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 18 Oktoba 2021, katika ziara yake ya kikazi wilayani Longido, Mkoa wa Arusha.

“Kuna vitendo vya watu kutowajibika kazini, wizi, upotevu wa mapato, uzembe bado mnaoneleana… shida hamchukui hatua, niombe halmashauri simamieni, piganeni na vitendo hivi. Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kasimamieni hayo,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewaagiza madiwani kusimamia mapato na matumizi ya fedha za halmashauri zao.

“Madiwani Serikali imebeba posho zenu, la kwenu kusimamia maendeleo, makusanyo na matumizi mazuri ya fedha nidhamu katika maeneo yenu,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!