Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia atumbua wakuu wa wilaya
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atumbua wakuu wa wilaya

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Julai, 2023 ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya ya Kilindi na Temeke na kuteua wengine wapya. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunusi, katika mabadiliko hayo madogo ya Wakuu wa Wilaya; Rais Samia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama


Pia metengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama. Amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.

Taarifa hiyo imesema, Rais Samia amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!