Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia: Athari za mabadiliko ya tabianchi hazichagui tajiri wala maskini
Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Athari za mabadiliko ya tabianchi hazichagui tajiri wala maskini

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema athari za mabadiliko ya tabianchi hazichagui nchi tajiri wala maskini hivyo kuna umuhimu kwa mataifa yote duniani kuwa na juhudi za pamoja kukabiliana na hali hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Novemba, 2021 wakati akihutubia mkutano wa Wakuu wa nchi wanaoshiriki mkutano wa 26 kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaofanyika huko Glasgow nchini Scotland maarufu kama COP 26.

Katika hotuba hiyo aliyotumia muda wa zaidi ya  dakika tatu, Rais Samia ameeleza namna mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri Tanzania katika ardhi ya uzalishaji mali, ongezeko la kina cha bahari, kuyeyuka kwa barafu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na namna ambavyo kisiwa cha Zanzibar kinavyoathirika kwa ongezeko la kiwango cha joto ambalo linaathiri ekolojia inayovutia watalii.

Aidha, ameongeza kuwa athari hizo zinatokea licha ya serikali kuendelea na azma yake ya kutenga hekta milioni 48 kwa ajili ya utunzaji wa misitu.

Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania inao mkakati maalumu wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambao umeainisha hatua kadhaa za kuchukua ikiwamo kupunguza athari za hewa ukaa kwa asilimia kati ya 30 na 35 ifikapo mwaka 2030.

Pia Rais Samia ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kuhimiza ahadi zao za kuratibu upatikanaji wa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 100 kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususani kwa nchi zinazoendelea.

Amesema athari zikitokea zitawakumba wote, nchi zilizoendelea kuwa athari zikitokea zitawakumba wote, nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!