Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateua majaji 52 ndani ya miezi 15
Habari za Siasa

Rais Samia ateua majaji 52 ndani ya miezi 15

Spread the love

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amesema ndani ya miezi 15 mahakama imepata ongezeko la majaji 52, tisa wakiwa wa Mahakama ya Rufaa na 43 wa Mahakama Kuu. Anaripoti Apaikunda Mosha TUDARCO … (endelea).

Jaji huyo ameeleza haya leo Jumatatu ya Tarehe 29, Agosti 2022 katika hafla ya uapisho wa majaji 21 wa Mahakama Kuu na Kamishna Jenerali wa Magereza iliyofanyika Ikulu Dodoma.

Amesema Rais Samia amevunja rekodi ya uteuzi wa idadi kubwa ya majaji ndani ya miezi 15 kuanzia mwezi Mei mwaka jana.

Amesema katika kipindi hicho amefanya uteuzi wa majaji saba wa mahakama ya rufani, majaji 21 wa mahakama kuu katika awamu ya kwanza na kwamba mwaka jana aliongeza majaji wawili wa mahakama ya rufani.

Amesema tarehe 6 mwezi huu ameteuwa majaji 22, “kwahiyo tumepata jumla ya majaji 52 ikiwa wa rufaa 9 na Mahakama Kuu 43.”

Amesema kwa muhimili wa mahakama uwezeshaji huo ni mkubwa na kwamba kuomgezeka kwa majaji tafsiri yake ni kusogeza huduma za utoaji wa haki karibu zaidi na wananchi.

Aidha amesema ongezeko hilo litasaidia kupunguza mzigo wa mashauri ambao majaji walikuwa wanaubeba kwa mwaka kwani kila jaji alikuwa na wastani wa mashauri 340 lakini kwa sasa wastani utashuka mpaka 265 kutokana na kuongezeka kwa nguvu kubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!