KATIKA kuadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 26 Aprili, 2022, Rais Samia Suluhu Hassan amesamehe wafungwa 3,826. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Rais Samia amechukua hatua hiyo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wafungwa hao wametokana na masharti 18 ya vifungo vyao.
Masharti hayo ni pamoja na wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu ambao wametumikia robo ya vifungo vyao na wapo kwenye ‘terminal stage’, ugonjwa huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa na wilaya.
“Wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao wametumikia robo ya vifungio vyao. Umri huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa au wilaya.
“Wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na watoto wanaonyonya, wasionyonya na wajawazito ambao wametumikia robo ya vifungo vya.
“Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili ambao wametumikia robo ya vifungo vyao. Ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa au wilaya,” imesema taarifa hiyo.
Wafungwa wengine ni waliohukumiwa aadhabu ya kuwekwa kizuizini ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka 10 na kuendelea.
Leave a comment