Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango: Muungano wetu ni zaidi ya hati, mambo ya muungano
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Muungano wetu ni zaidi ya hati, mambo ya muungano

Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango, amesema ushirikiano na mwingiliano wa wananchi wa pande zote za muungano unadhihirisha kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni zaidi ya hati ya muungano na orodha ya mambo ya muungano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Mpango ameyasema hayo leo tarehe 26 Aprili, 2022 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika Dodoma.

Amesema wananchi wa pande mbili wamepiga hatua kubwa na kasi ya ushirikiano imeongezeka, “wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara wa pande zote wameonesha kuwa Muungano wetu ni zaidi ya hati ya makubaliano ya Muungano na orodha ya mambo ya Muungano.”

Ameongeza kuwa ushirikiano umeongezeka na wananchi wamejenga mshikamano, udugu, ushirikiano katika huduma, ubadilishanaji wa bidhaa na kutegemeana katika nyanja zote.

“Sisi sote ni mashahidi kuwa muungano wetu umekuwa na manufaa makubwa kisiasa na kijamii. Muungano umesaidia kujenga Taifa moja lenye watu wamoja wanaozungumza lugha moja,”

Akitaja bbaadhi ya mafanikio ya Muungano, Dk. Mapngo amesema kabla ya muungano na muda mfupi baada ya kuungana kulikuwa na Sheria mbili tofauti za uraia na uhamiaji, “jambo la kujivunia sasa masuala haya yanasimamiwa na sheria moja.”

Amesema kutokana na kuwa na uraia wan chi moja wananchi wamekuw ana uwezo wa kwenda au kuishi sehemu yeyote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila vikwazo.

“Mfano ukienda Sumbawanga utawakuta Wapemba na ukienda Unguja utawakuta Wachaga, Wamasai, Wasukuma n.k kumekuwepo mwingiliano wa utamaduni kama aina ya vyakula mitindo ya mavazi na burudani na kuoleana pande zote za Muungano,” amesema na kuongeza “mambo haya yamepelekea wananchi kuwa wamoja zaidi,” amesema Dk. Mpango.

Mbali na hayo amesema pia kuna muingiliano katika mambo ya kisiasa na kiutawala ikiwemo viongozi wa juu wa vyama vya siasa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka katika pande zote za muungano, “kwakweli hili ni jambo la kujivunia sana,”

Jambo lingine amesema ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi katika kioindi chote cha miaka 58 imeendelea kuimarika “ambapo sote tunafurahia uwepo wa utulivu na amani nchini ambao umewawezesha wananchi wetu kuendelea na shughuli zao za kiuchumi, kisiasa na kijamii.”

Amesema pande zote za muungano zimeweza kulinda uhuru (Tanganyika) na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar dhidi ya vitisho mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!