Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia asaini miswada sheria za uchaguzi licha ya kelele za wapinzani
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia asaini miswada sheria za uchaguzi licha ya kelele za wapinzani

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesaini miswada ya sheria za uchaguzi kwa ajili ya kuwa sheria kamili na kuanza kutumika, licha ya kelele za wapinzani zilizomtaka asisaini ili ifanyiwe marekebisho hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 2 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.

“Katika mkutano wa 14 wa Bunge, Bunge lilipitisha miswada minne ya sheria na kwa taarifa hii napenda kulitaarifu Bunge kuwa tayari miswada hiyo minne imepata kibali cha Rais Samia na kuwa sheria za nchi, kwa hiyo zimeshakua sheria kamili na Rais ameshafanya kwa sehemu yake,” amesema Spika Tulia.

Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa 2023 umesainiwa na kuwa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 1 ya 2024. Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa 2023 umekuwa Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Namba 2 ya 2024.

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa 2023, umekuwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa namba 3 ya 2024 na muswada wa mwisho uliosainiwa umekuwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 4 ya 2024.

Miswada hiyo imesainiwa katika kipindi ambacho baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kikimtaka Rais Samia asiisaini ili ifanyiwe marekebisho kwa madai kuwa ina dosari ambazo hazitatatua changamoto za kiuchaguzi.

Hata hivyo, Serikali imekuwa ikisema miswada hiyo ina lengo la kuhakikisha upatikanaji wa chaguzi huru na za haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

error: Content is protected !!