Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mzee Makamba aichambua CCM ya Samia
Habari za Siasa

Mzee Makamba aichambua CCM ya Samia

Spread the love

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuph Makamba, amesema chama hicho chini ya uongozi wa mwenyekiti wake taifa, Dk. Samia Suluhu Hassan, itapata mafanikio. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es salaam…(endelea).

Mzee Makamba alitoa kauli hiyo jana tareje 1 Aprili 2024, nyumani kwake jijini Dar es Salaam, alipotembelewa na Katibu Mkuu mpya wa CCM, Balozi Emmnaule Nchimbi.

“Chini ya uongozi wako (Balozi Nchimbi) na wa mama Samia, makamu mwenyekiti CCM bara, Abdulrahman Kinana na Mwinyi (makamu mwenyekiti CCM Zanzibar), CCM itapata mafanikio,” alisema Mzee Makamba.

Kauli hiyo ya Mzee Makamba imekuja katika kipindi ambacho CCM kuna panga pangua ya viongozi wake kwa ajili ya kupata safu mpya ya viongozi. Viongozi wa chama hicho walioondolewa katika nafasi zao baada ya kupata teuzi serikalini ni aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda, aliyeteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wengine waliondolewa CCM ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Gilbert Kalima, aliyeteuliwa na rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Raphael Lulandala, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Licha ya kutaja namna Rais Samia na wasaidizi wake wataipa mafanikio chama chake, kiongozi huyo wa CCM imejipambanua kwa kuvunja makundi ya ndani  ili kuimarisha umoja na mshikamano kuelekea chaguzi zijazo.

1 Comment

  • Huyu hatumuamini yeye na kundi lake.
    Kama ulikataliwa na JPM hakuna wakukuamini.
    Nivyema tuwaachie waliopo wafanye kwa maono yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!