Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apangua wakuu wa mikoa, wilaya
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia apangua wakuu wa mikoa, wilaya

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi pamoja na makatibu tawala. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka leo Jumamosi tarehe 9 Machi 2024.

Katika uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, wakati aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Luteni Patrick Kena Sawala akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Paul Matiko Chacha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Tabora, akitokea nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.

Katika mabadiliko hayo madogo ya wakuu wa mikoa na wilaya, Rais Samia amewahamisha wakuu wa mikoa wanne, ambao ni Ahmed Abbas Ahmed aliyehamishiwa Mkoa wa Ruvuma akitokea Mtwara. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amehamishiwa Iringa.

Wengine waliohamishwa ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Batilda Salha Burian, kwenda Mkoa wa Tanga na Halima Dendego, aliyehamishwa kutoka Iringa kwenda Singida.

Kwa upande wa wakuu wa wilaya, Rais Samia ameteua watano ambao ni Abdallah Nyundo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Festo Kiswaga (Monduli), Evans Mtambi (Mkinga), Almishi Hazali (Hanang’) na Joachim Nyingo (Kilolo).

Wakuu wa Wilaya waliohamishwa ni 25 akiwemo Deusdedith Katwale, amehamishwa kutoka Wilaya ya Chato kwenda Wilaya ya Tabora.

Janeth Mayanja amepelekwa Wilaya ya Chamwisho akitokea Hanang’ na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julisu Mtatiro, amehamishiwa Wilaya ya Shinyanga.

Makatibu Tawala saba nao wameguswa katika mabadiliko hayo, akiwemo Toba Alnason Nguvila, aliyehamishwa akutoka Mkoa wa Kagera kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam.

Aliyekuwa Katibu Tawala Ruvuma Stephen Ndaki, amepelekwa Kagera naRehema Madenge amehamishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Ruvuma.

1 Comment

  • Wachape kazi kimaadili kiujuzi kitaaluma ili ziwe na matokeo. Siasa tu matokeo yake ni manenoneno tu hayashikiki ni hamasa zaidi kuliko productivity. Sifa stahiki kwa kila kazi ni kigezo kikuu bila sifa ni kujiabisha katika dunia Simi. Kamishna ni cheo kikuu sio Cha kisiasa Hilo jina kamishna ni ukamishna hasa kwa sifa madhubuti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!