Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ma-RC waliopigwa panga hawa hapa
Habari za Siasa

Ma-RC waliopigwa panga hawa hapa

Kanali Laban Thomas
Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo wakuu wa mikoa na kuwaacha kando watatu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Col. Ahmed Abbas Ahmed

Walioachwa ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba ambaye nafasi yake imechukuliwa na  wa Dk. Batilda Buriani aliyetokea Tabora. Hata hivyo, Kindamba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na kuchukua nafasi ya Gilliard Wilson Ngewe ambaye atapangiwa kazi.

Kanali Laban Thomas aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma naye panga limemkuta baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Col. Ahmed Abbas Ahmed aliyehamishwa kutoka Mtwara.

Naye Dk. Fransis Michael aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Songwe pia nafasi yake imechukuliwa na Daniel Chongolo aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM aliyejiuzulu wadhifa huo mwaka jana.

2 Comments

  • Namfahamu vzr Dk Michael ni mchapa kazi mahiri, muwazi, mwenye uwezo Kama Katibu Mkuu na au Mtendaji mkuu wa taasisi yenye kuleta matokeo makubwa. Siasa hasha.

  • Nimefurahi sana kwa Daniel chongolo kurudi shwa! Daa huyu baba aliniuma sana moyo kwa kujiudhuru uongozi! Mungu mkubwa! Pongezi sana q kwako Mwanamke Jasiri,mwenye kuipambania Nchi yetu,usiyeyumba,Mama bora mwenye kuyaweka moyoni bila kukasirika juu ya Matusi ,kebehi za wapinga ubora wa majitoleo yako kwa Taifa letu ,Mama Samia Rais wangu Mungu akutetee na akutie nguvu🙏🙏🙏♥️♥️♥️

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!