Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Mwinyi kuwawezesha wasaidizi kisheria
Habari Mchanganyiko

Rais Mwinyi kuwawezesha wasaidizi kisheria

Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ameahidi kutoa majengo na usafiri wa bajaji, kwa wasaidizi wa kisheria ili waweze kufikisha huduma hiyo kwa wananchi wenye uhitaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ametoa ahadi hiyo leo Jumamosi, akifunga maadhimisho ya nne ya wiki ya msaada wa kisheria visiwani humo.

Rais Mwinyi amesema Serikali yake itatekeleza ahadi hiyo haraka iwezekanavyo, ili kuwezesha huduma kufika kwa wakati kwa wananchi lengo likiwa ni uimarishaji upatikanaji haki kwa wasio na fedha.

“Nimeelezwa kuwa wasaidizi wa kisheria wanahitaji majengo ya ofisi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zao vizuri.  Lakini pia wanaomba usafiri wa bajaji, hawa watu hawana makubwa pengine wangetaka kuomba magari,” amesema Rais Mwinyi na kuongeza:

“Hivyo, mie nalichukua na Serikali inakwenda kulishughulikia haraka.  Najua tuna mambo mengi lakini ni muhimu sana kwa ajili ya kujenga mazingira bora ya wao kutekeleza majukumu yao.”

Rais Mwinyi ametoa ahadi hiyo baada ya mwakikishi wa wasaidizi wa kisheria, Salehe Mussa Alawi, kuomba Serikali yake kuwasaidia majengo ya Ofisi na usafiri kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi, hasa wa maeneo ya pembezoni.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Legal Service Facility (LSF), Jaji Mstaafu, Robert Makaramba, amesema wasaidizi wa kisheria ni nyenzo muhimu katika kuzisaidia Serikali kuboresha sekta hiyo.

“Suala hili linaanza na uboreshaji wa mifumo, miundo, sera na sheria zitakazohakikisha huduma za msaada wa kisheria zinatolewa katika hali endelevu kupitia uwezeshaji wa Serikali kwa kushirikiana na watoa msaada wa kisheria,” amesema Jaji Makaramba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!