Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Raila akinukisha tena Kenya “wakati wa mazungumzo umekwisha”
Kimataifa

Raila akinukisha tena Kenya “wakati wa mazungumzo umekwisha”

Raila Odinga
Spread the love

 

KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ametimiza azma yake ya kuitisha maandamano kwa ajili ya kupinga muswada mpya wa sheria ya fedha, uliosainiwa hivi karibuni na Rais wa taifa hilo, William Ruto.

Odinga amedai kuwa muswada huo unaongeza maumivu ya gharama za maisha kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza wakati wa maandamano hayo, yaliyopewa jina la sabasaba, leo tarehe 7 Julai 2023, Odinga amedai ameamua kuyaitisha baada ya Serikali ya Ruto kukaidi wito wa kupunguza gharama za maisha na maboresho katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC).

Kiongozi huyo wa upinzani amedai, Rais Ruto amekiuka ahadi aliyoiweka kwa wananchi na hivyo atawaongoza katika mapambano ya kurejesha mamlaka yao “tunaanza harakati ya kuchukua mamlaka moja kwa moja.”

“Tumeongea vya kutosha, jamaa walituambia tupoze moto tuzungumze tukakubali kwa moyo mkunjufu, tukasema tuko tayari wakatoa watu saba na sisi tukatoa saba tukakubali kuwa wajinga na wakasema watatekeleza mambo matatu, muhimu la kwanza gharama ya maisha kurudi chini lakini wamezidisha kuliko kupunguza, ushuru wamepandisha zaidi,” amesema Odinga.

Katika hatua nyingine, Odinga amedai kuna njama za kukiua chama chake cha Azimio, kwa kuwachukua wabunge wake, huku akisema hatua hiyo haitamaliza nguvu yao kwa kuwa inatoka kwa wananchi.

Maandamano hayo yameitikiwa na wafuasi wa Odinga katika maeneo mbalimbali Kenya, ikiwemo Kisii, Mombasa, Nairobi na Kisumu.

Baadhi ya wanawake katika Mji wa Kisii walioingia barabarani kuandamana, waliwasha moto wa kuni kisha kuweka sufuria na kuanza kupika maji wakiashiria kukosekana kwa vyakula.

Askari Polisi wameonekana wakitanda katika mitaa ambayo wafuasi wa Odinga wanafanya maandamano, huku baadhi ya maeneo wakipiga mabomu ya machozi.

Odinga amewataka wafuasi wake kufanya maandamano ya amani pasina kuharibu mali za watu, huku akiwataka Polisi kutowafanyia fujo.

Pia, ameanzisha zoezi la wafuasi wake kukusanya saini zao ili zifike milioni 10, kwa lengo la kutuma ujumbe kwa Rais Ruto, kwamba wanapinga uamuzi wake wa kusaini sheria inayodaiwa kuongeza ugumu wa maisha.

Hii si mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo wa upinzani kuitisha maandamano, mapema Machi 2023, aliitisha tena yasiyo na kikomo lakini Serikali ya Ruto ilimwita mezani kwa ajili ya mazungumzo, kisha akasitisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!