MATAIFA manne ya kiarabu, yanayoongoza masharti makali dhidi ya Qatar, yanasema kuwa, hatua ya Doha kukatalia mbali masharti hayo magumu dhidi yake, inaashiria nia yake ya kuendeleza sera ya kuhujumu usalama, katika eneo la mataifa ya Ghuba, anaandika Hamisi Mguta.
Kupitia taarifa ya pamoja, Saudia , Milki za kiarabu Misri na Bahrain, zimeonya kuwa, zitatoa hatua nyingine mpya na ngumu zaidi dhidi ya Qatar.
Mataifa hayo manne yalikatisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar mwezi uliopita, yakidai kuwa, taifa hilo linafadhili makundi ya kigaidi duniani, kama vile kundi la Muslim Brotherhood nchini Misri, na linashirikiana na hasimu mkuu wa Saudi- Iran.
Rex Tillerson, Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani, anasafiri hadi Kuwait kujadili namna ya kutanzua mtafaruku huo.

Qatar imerudia mara kadhaa kuwa, orodha ya masharti hayo, hayana maana kabisa, mojawepo ikiwa kufunga shirika lake la habari la Al Jazeera.
Leave a comment