Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Sherehe za miaka 60 tangu Aga Khan kusimikwa uimamu kuanza kesho
Habari Mchanganyiko

Sherehe za miaka 60 tangu Aga Khan kusimikwa uimamu kuanza kesho

Spread the love

KESHO kunatarajiwa kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangu  Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa imamu Mkuu wa dhehebu la Shia Ismailia ulimwenguni, tukio ambalo lilitokea tarehe 11 Julai, 1957, anaandika Pendo Omary.

Pia, maadhimisho yataenda sambamba na kutambua shughuli za maendeleo zinazofanywa na Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN).

Maadhimisho hayo yatafanyika kwa siku tatu ambapo Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe hizo mnamo tarehe 9 Julai, 2017.

Profesa Joe Ligalla, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan amesema “katika sherehe hizi, tunataka wananchi watambue kwamba kuna mambo mengi yamefanyika kupitia mtandao wa maendeleo wa Aga Khan.

“Si sherehe za kusherehekea tu mtu kuwa Imamu wa kidini lakini tutambue kuwa ni kiongozi aliyeshiriki katika kubuni miradi ya kimaendeleo hapa Tanzania.”

Aidha, AKDN umefanya kazi kubwa ya kuwainua wananchi wa kiapato cha chini  na kutoa huduma katika sekta za afya, elimu, kilimo, bima na utalii.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!