August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lipumba, Maalim Seif siku zinahesabika

Spread the love

KESI ya Madai Na. 21 ya mwaka 2017 iliyopangwa kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera kuhusu wizi wa Sh. 369 milioni, fedha za ruzuku za Chama cha Wananchi – CUF imeahirishwa mpaka tarehe 10, Julai 2017, anaandika Hamisi Mguta.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Bodi ya wadhamini wa CUF, ambapo  watuhumiwa ni pamoja na Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa huku akiwa amefukuzwa uanachama na CUF.

Katika kesi hiyo jopo la mawakili wa upande wa mashtaka linaongozwa na Juma Nassoro, Daim Halfan na Hashimu Mzirai, upande wa utetezi unawakilishwa na mawakili ni Gabriel Malata ambaye ni Wakili wa Serikali Mkuu na Makubi Kunju, wakili wa upande wa Lipumba.

error: Content is protected !!