Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Simanzi mazishi ya Shaban Dede
BurudikaRipoti

Simanzi mazishi ya Shaban Dede

Marehemu Shaaban Dede
Spread the love

HAKIKA ni simanzi na majonzi ndivyo vimetawala kwa wadau wa mziki wa dansi Tanzania kufuatia kifo cha Shaban Dede, Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi huku mamia wakiwa wamejitokeza katika mazishi yake katika mabauri ya Kisutu jiji Dar es Salaam, anaandika Hamisi Mguta.

Dede amefariki dunia asubuhi ya jana Julai 6 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa akipatiwa matibabu akisumbuliwa na maradhi ya sukari pamoja na figo.

Alikuwa akiitumikia Bendi ya Msondo Music lakini huko nyuma aling’ara katika Bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee.

Kupitia muziki wake, Dede alipachikwa jina la ‘Kamchape’ na mashabiki zake, akiwa hodari wa kutunga na kuimba nyimbo za maudhui na ujumbe mzuri katika jamii.

Bendi aliyodumu nayo kwa kipindi kirefu katika maisha yake ni Msondo Ngoma ambapo hadi kifo kilimkuta akiwa katika bendi hiyo, alikuwa kiongozi pamoja na  Saidi Mabera ambaye  ni Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo.

Said Mabera, Mkurugenzi wa Bendi hiyo akizungumza katika mazishi hayo Makaburi ya Kisutu amesema kikubwa kitakachomfanya kumkumbuka Dede ni namna ya utunzi wake ulivyo na jumbe nzuri.

“Alikuwa mwenzetu kwa muda mrefu katika bendi ya Msondo Ngoma, alikwenda Juwata na baadaye akaenda sikinde lakini baadaye tukakubaliana akarudi tena Msondo.

“Amefariki akiwa kwenye bendi ya Msondo Ngoma na tutamuenzi kwa kumkumbuka kwa alichotufanyia katika bendi yetu ya msondo ngoma,” amesema Mabera.

Said Mabera, Mkurugenzi wa Bendi Msondo Ngoma akizungumza na waaandishi wa habari muda mfupi baada ya mazishi ya Marehemu Shaban Dede aliyekuwa mwanamuziki katika bendi hiyo

Hata hivyo, Waziri Ally , ambaye ni Mwimbaji katika bendi ya Njenje amesema kuwa anamkumbuka Dede kwasababu alikuwa rafiki wake wa kwanza wakati alipohamia katika Bendi ya Msondo.

“Mimi na shaban tulikutana na kufahamiana mwaka 1979 na nilikaa naye vizuri sana kwasababu wakati naingia bendi ya Msondo rafiki yake wa kwanza ni mimi. Nitamkumbuka sana wimbo wake wa kwanza kutunga unaitwa fatuma kwasababu  mimi ndio wakwanza kuniimbia kabla hajautoa.

“Uwezo wake wa utunzi ni kitu bambacho sitoweza kusahau na nyimbo zake nyingine ukisikiliza ujumbe wake hadi sasa unaleta maana,” amesema Ally.

Hata hivyo, Ally ametoa rai kwa Wanamuziki wanaochipukia wajifunze kutoka kwa marehemu kupitia utashi wake wa utunzi na kuimba.

Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze amesema, aliishi na marehemu kama mjomba kutokana na historia ya wazazi wake ambapo wakati wa uhai wake alikuwa abagui wa kukaa na kuzungumza naye.

“Mimi kwanza nitoe salamu za pole kwa familia ya wapenda mziki na wana Dar es Salaam lakini binafsi nimeguswa na msiba huu kwasababu Dede nimefahamiana naye kama Mjomba kutokana  na wazazi wetu.

“Kubwa zaidi ni yeye alivyoweza kuishi maisha yake, aliishi maisha ya aina nyingi, hapa nazungumzia sana maisha ya nje ya jukwaaa kwasababu alikuwa mtu wakipekee ukikutana naye anakufanya uonekane unaendana na umri wake,” amesema.

Dede, alishirikiana kuimba katika Bendi ya Msondo na waimbaji Juma Katundu, Twaha Mohamed, Hassan Moshi William ‘TX Junior’ na Hussein Kalembo na nyimbo Nyimbo alizotunga ni nyingi na alizoimba pia ni nyingi kama vile ‘Kilio Cha Mtu Mzima’, ‘Kaza Moyo’ (Msondo), ‘Diana’, ‘Tui la Nazi’, ‘Amina’ (Sikinde), ambazo zinaonesha uhalisia wa maisha ya watu na zilijizolea umaarufu katika kumbi mbali mbali za muziki na kuvuta mashabiki wa rika zote.

Hata hivyo, Dede aliwahi kufanya kazi na  baadhi ya wanamuziki ambao wamekwisha fariki akiwemo Mzee Muhidini Gurumo. Wengine ni TX Moshi William, Nicko Zengekala, Selemani Mbwembwe, Joseph Maina, Mustafa John Ngosha, Suleimani Mwanyiro, Tino Maselenge ‘Arawa’,  Athuman Momba na mpulizaji wa saxophoni Alli Rashidi aliyefariki dunia siku ambayo bendi hiyo ikitimiza miaka 50, Oktoba 10, 2014.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala...

error: Content is protected !!