Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari Profesa Mkumbo awasha moto bungeni bei mafuta
HabariHabari za Siasa

Profesa Mkumbo awasha moto bungeni bei mafuta

Prof. Kitila Mkumbo
Spread the love

 

MBUNGE wa Ubungo, Profesa Kitiola Mkumbo amewasha moto bungeni kutokana na Serikali kutochukua hatua yeyote juu ya kupanda bei ya nishati ya mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Amesema kutoa sababu za kupanda kwa bei haitoshi kumsaidia Mtanzania kupunguza makali ya maisha yanayotokana na kupanda kwa bei hizo.

Prof, Mkumbo ametoa maoni hayo leo Ujumaa tarehe 8 Aprili wakati akichangia hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2022/23.

Amependekeza kupunguzwa kwa tozo za mafuta kwa angalau Sh 300-400 kwa kipindi fulani cha muda huu ambao bei zimepanda kwenye soko la dunia.

Ameongeza kuwa ili kufidia fedha zitakazopotea kutokan na kuondoa tozo hizo, Serikali ikope kufidia ili miradi ya maendeleo isikwame.

“Hiki sio kiwango cha kawaidia cha upandaji wa bei ya mafuta na tunafahamu sio kwa sababu ya Serikali lakini hoja ya msingi Serikali inachukua hatua gani kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha.

“Mapendekezo yangu ni kwamba katika zile levy Sh 792 ambazo zinakusanywa Kamati ya bajeti inaweza kushauri tukachukua Sh 300 hadi 400 kwa kipindi cha miezi mitatu au minne hadi hali itakavyokaa sawa.

“Inapofika wakati wananchi wanaumia msemaji wao mkubwa ni bunge. Haliwezi kukaa kimya na kuridhika kwa maelezo ya Serikali kwamba mafuta yamepanda kwasababu hizi na hizi hizi, hii haitoshi muhumimu ni kwa namna gani tunamsaidi mwananchi,” amesema Mkumbo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!