Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Prof. Ndalichako aipa rungu TCU wanaowasajilia vyuo waombaji
Elimu

Prof. Ndalichako aipa rungu TCU wanaowasajilia vyuo waombaji

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako
Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu nchini humo (TCU) kuwachukua hatua taasisi au mtu binafsi wanaowasajilia vyuo waombaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, kitendo hicho hakikubaliki kwani kinawanyima uhuru waombaji wa kuchagua vyuo wanavyovipenda.

Profesa Ndalichako hayo jana Alhamisi, tarehe 7 Oktoba 2021, jijini Dar es Salaam,
wakati akifungua mkutano wa kubadilishana uzoefu kati ya TCU na wenyeviti wa mabaraza ya vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki.

Alisema kunahitajika umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi na uendeshaji wa vyuo hivyo ili kufikia lengo hilo.

Katika maelezo yake, Profesa Ndalichako aliwataka wenyeviti wa mabaraza ya vyuo hivyo kusimamia kikamilifu uendeshaji wa vyuo vyao ili kuhakikisha wanapunguza changamoto zilizopo.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo ni upungufu wa wahadhiri wenye sifa stahiki, kutolipa wafanyakazi mishahara na stahiki nyingine, kuwepo kwa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia isiyokidhi viwango pamoja na ucheleweshaji wa matokeo ya mitihani.

“Kuna baadhi ya vyuo haviwalipi wafanyakazi hadi inapelekea wao kushikilia karatasi za mitihani ya wanafunzi na hivyo kuwanyima wanafunzi haki ya kupata matokeo yao kwa wakati. Hii si sawa kwa kuwa tunakuwa tunawaandaa wahitimu ambao wanatoka chuoni wakiwa na hasira na hivyo baadae kupata watendaji wasio na maadili bora,” alisema Profesa Ndalichako.

Aidha, Profesa Ndalichako alimpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwezesha upatikanaji wa mkopo nafuu wa zaidi ya Sh.972 bilioni kutoka Benki ya Dunia (WB) utakaotumika kuimarisha elimu ya juu ambapo jumla ya vyuo 14 vitanufaika na kupunguza changamoto ikiwemo ya miundombinu.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia 27 Mei mwaka huu imesaini mradi wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 425, sawa na Sh.972 bilioni kwa ajili ya kuimarisha elimu ya juu.”

“Haijawahi kutokea katika historia ya Nchi yetu kuweza kupata fedha nyingi kiasi hicho hivyo nimpongeze sana Rais wetu kwa kuwezesha hilo,” alisema Profesa Ndalichako.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe alisisitiza umuhimu wa menejinenti za vyuo vikuu kusikiliza na kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wanafunzi vyuoni badala ya kuyapuuza na hatimaye malalamiko hayo kuletwa wizarani.

Alisema kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya vyuo kuchelewa kuwapa wanafunzi fedha za mikopo na kuwataka kuteua maafisa mikopo wenye uwezo ili kupunguza malalamiko hayo.

“Baadhi ya vyuo vinachelewa kupeleka stakabadhi ya malipo bodi ya mikopo hadi inafika wakati wa mitihani bodi inakuwa bado haijafanya malipo, matokeo yake vinawazuia wanafunzi kufanya mitihani au kuwafungia matokeo yao. Hii si sahihi, mnatakiwa mpeleke stakabadhi hizo kwa wakati,” alisema Profesa Mdoe.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Prof. Lugano Kusiluka alikiri kupokea ushauri na maelekezo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha utendaji kazi na kupunguza malalamiko na changamoto zilizopo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

error: Content is protected !!