June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Achana na Arnold, huyu ndiye jabali mwenye nguvu zaidi duniani

Hafthor Julius Bjornsson

Spread the love

 

HAFTHOR Julius Bjornsson ndiye mwanaume mwenye nguvu zaidi duniani ambaye pia ni mcheza filamu nchini Marekani. Ni raia wa Iceland, alipata umaarufu zaidi baada ya kuwa mmoja kati ya washiriki kwenye filamu ya “Game of Throne.”

Amevunja rekodi na kutwaa ubingwa mara tatu mfululizo ndani ya mwaka mmoja (2018). Mwaka 2020 alikuwa na uzito wa kilogram 501. Kutokana na ukubwa wa mwili wake pia anajulikana kama “The Mountain”

Ametwaa ubingwa na kuwa mwanaume mwenye nguvu Barani Ulaya (Europe Strongest Man), pia amekuwa mwanaume mwenye nguvu duniani baada ya kushinda tuzo ya ‘World’s Strongest Man.

Kwa mara ya tatu akawa mshindi kwenye mashindano yaliyoandaliwa na aliyekuwa Gavana wa jimbo la Carfonia na mcheza filamu wa zamani, Arnold Schwarzenegger, yanayojulikana kama Arnold Strongman Classic.

Ingawa ana mwili mkubwa na ni mrefu wa kimo lakini ana mwanamke mwenye mwili mdogo.

Kelsey Henson ndilo jina la mkewe. Mwanamke huyo ni maarufu kwa ujuzi wake kwenye mitandao ya kijamii ambao ni mkufunzi wa mazoezi ya viungo.

Makala hii imeandaliwa na Victoria Mwakisimba.

error: Content is protected !!