December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wauwa majambazi watatu

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Kigoma limewauawa watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi huku wengine wawili wakitorokea kusikojulikana. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumzia kuhusu tukio hilo lililotokea jana, Kamanda wa Polisi Kigoma, Martin Ottieno amesema majambazi hao waliuawa wakati wa majibizano ya risasi baina yao na askari polisi katika msitu wa Muyovosi walikokimbilia baada ya kufanya tukio la uporaji.

Kamanda Ottieno ameeleza kuwa, majambazi hao walitokomea katika msitu wa Muyovosi baada ya kutekeleza tukio la uporaji katika Kijiji cha Nyarulanga wilayani Kibondo, kwa kutumia silaha kwa watumishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi la Good Neighbour na kuwapora mali zao ikiwemo fedha na kompyuta mpakato (Laptop).

Amesema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za tukio hilo, polisi walifanya masako na kufanikiwa kuwakuta majambazi hao kwenye msitu wa Muyovosi, na kwamba baada ya majambazi hao kuwaona polisi walianza kufyatua risasi, ndipo majibizano ya risasi yalipoanza.

“Kuna majambazi wanaosemekana zaidi ya watano, walikuwa barabarani wakasiammisha hiace moja na Landcruiser la shirika linalotoa huduma kwa wakimbizi la Good neighbour  wakapora vitu mbalimbali  pamoja na hela za abiria waliokuwepo ndani ya gari, walielekeea msitu wa Muyovosi,” amesema na kuongeza Kamanda Ottieno.

“Tulifika eneo hilo majira ya saa kumi na mbili jioni tukafanikiwa kukutana na wale majambazi wakaanza kuturushia risasi, kutokana na umahiri wa vijana wetu walifanikiwa kupambana na majambazi wale watatu tukafanikiwa kuwaua pale pale na kuokoa mali za abiria walioporwa katika eneo hilo.”

Kamanda Ottieno amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka majambazi waliotoroka.

error: Content is protected !!