Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wasonga atamani kuvaa viatu vya Fatma Karume
Habari Mchanganyiko

Wasonga atamani kuvaa viatu vya Fatma Karume

Spread the love

WAKILI wa Kujitegemea Godfrey Wasonga ametangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Urais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) huku akitangaza kufanya ushawishi wa kubadilisha katiba ya Jamhuri ya Tanzania. Anaripoti Danson Kaijage

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya nia yake ya kugombea nafasi hiyo Wasonga alisemakuwa kati ya jambo ambalo atalipogania ni kuhakikisha anatumia nafasi yake kufanya ushawishi wa kubadilisha katiba ya Tanzania ili kuondoa sheria kandamizi.

Wakili huyo wa kujitegemea alisema kuwa kwa sasa hakuna demokrasi ya kweli kutokana na kuwepo kwa katiba iliypitwa na wakati ambayo kwa sasa haiendani na matakwa ya sasa ya kidunia.

“Ikumbukwe kuwa katiba tuliyonayo kwa sasa ni ya mw aka 1964 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1977  ambayo kwa sasa haiwezi kuendana na matakwa ya kidunia.

“Kama hakuna katiba yenye kurekebishwa na kuondoa sheria kandamizi hatuwezi kuwa na demokrasia ya kweli na tukiwa na katiba nzuri itaweza kumsiadia hata rais aliyepo madarakani” alisema Wasonga.

Katia hatua nyingine wasonga alisema kuwa iwapo atapata nafas ya kuwa rais atakuwa na vipaumbele vitano ambavyo ni kubadilisha katiba ya TLS kutoka kufanya uchaguzi kwa mwaka mmoja na kuwa miaka miwili.

Kipaumbele kingine ni kuboresha huduma kwa wanachama hasa katika bima ya Afya ili kila wakili awe na bima ya afya ili iweze kumsaidia yeye na familia yake.

Alisema kipaumbele kingine ni kuondoa kipengele cha ulipaji wa ada ambayo ulipwa kila mwisho wa mwaka na badala yake iwe inalipwa mwanzo wa mwaka au wakati wowote na siyo lazima mwisho wa mwaka.

Aidha alisema kuwa katika uongozi wake atakuwa na sera ya pensheni kwa mawakili ambao watakuwa wamefikia uzeeni ili awe na kitu ambacho kitaweza kumsaidia.

Aidha alisema kuwa ada za mawakili zimekuwa zikiongezeka kutoka sh.30000 kufika sh.50000  na ili uweze kufika katika vikao vya mawakili ni lazima ulipe kiasi cha sh.120,000  lakini katika uongozi wake ataishusha hadi kufikia kiasi cha sh. 60000 kama ilivyokuwa awali ili kumpunguzia mwanachama badala ya kumuongezea gharama.

Wasonga alisema kuwa kero ambazo zinawasumbua Mawakili ni semina ambazo zimekuwa ni ghari  ambazo ni sh 60000 hadi 130,000  kutokana na hiyo mwanachama atatakiwa kulipa 100,000 kwa mwaka ambazo zitafunguliwa akaunti maalum ili kumwezesha mwanachama kujua anataka kwenda semina ipi.

 Wakili huyo alisema kwamba katika uongozi wako atatoa elimu juu ya ujasiriamali ambao utaweza kumsaidi wakili pale ambapo hatakuwa hana kazi kwa maana ya kutokuwa na mteja ataendelea na shughuli nyingine ya kumingizia kipato.

“Wapo Mawakili wachanga ambapo wanahitaji kuboreshewa mazingira ikiwa ni namna gani ya kuweza kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika mabenki au akiwa mwanachama anaweza kukopeshwa moja kwa moja kutoka katika mfuko wa chama cha Mawakili.

Jambo lingine ni kutoa taarifa kwa wakati kwani kwa sasa Mawakili wengi hawapati taarifa na wakati mwingine wakizidai wanachukua muda kuzipata lakini kwa uongezi wake ameeleza kuwa kila kikao watu watapata taarifa.

Kipengele kingine ni mahusiano kani kwa kumekuwepo kwa mahusiano mabaya kati ya TLS, Serikali na Bunge.

“Kwa uongizi wangu kama nitachaguliwa kitu ninachokitegemea ni kupata mahusiano mema kati ya mihilimi hiyo pamoja na kujenga mahusiano na jamii kwa ujumla pamoja na kushirikiana na vyama mbalimbali vya mawakili duniani” alisema Wasonga.

“Katika kipindi change nitafanya uwekezaji na tufike hatua kutambua kuwa wadau wetu ni mahakama, serikali na Bunge na kutokana na hilo tutawekeza kwenye ardhi ili kuonesha na kutafuta fursa kutokana na serikali kuhamia Dodoma.

“Kutokana na hali hiyo wataweza kujenga majengo ya kitega uchumi ikiwa ni pamoja na kuachana na kukodisha kumbi na badala yake tuweze kutumia majengo yetu huku kuona namna gani ya kila mkoa kuwa na ardhi ambayo itaweza kuingiza kipato kwa TLS”  alisema wakili Wasonga.

Kwa mujibu wa Wasonga alisema kuwa mchakato wa kuanza harakati za kusaka kura unaanza 13 Machi  na uchaguzi unatarajiwa kufanyika 6 Aprili mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!