December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamati za Bunge kufanya mapitio Bajeti 2019/20

Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

KAMATI za Bunge la Jamhuri zitaanza kuketi leo tarehe 12 Machi 2019 kufanya kazi mbalimali ikiwa ni pamoja na kupitia matumizi ya Fedha za Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/19. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa, pamoja na mapitio ya bajeti inayokwenda ukingoni (2018/19) pia vikao hivyo vitapata fursa ya kupitia makadirio ya fedha za bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Pia kamati hizo zitafanya ziara kupita na kukagua miradi mbalimbali ili kuangalia uwekezaji na kujiridhisha thamani ya matumizi ya fedha za umma na matumizi yake.

Vikao vya kamati hizo vitachukua jumla ya siku 18 ambapo vitakoma tarehe 30 Machi 2019 kabla ya kuanza kwa Bunge la Bajeti 2019/20 tarehe 2 Aprili 2019.

error: Content is protected !!