Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi watoa kauli madai mauaji Kibiti kuibuka tena
Habari za Siasa

Polisi watoa kauli madai mauaji Kibiti kuibuka tena

Spread the love

JESHI la Polisi nchini, limewataka wananchi wapuuze madai ya mauaji ya watu wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, kuibuka tena, likisema hali ni shwari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taraifa hiyo imetolewa leo na Jeshi la Polisi kuoitia ukurasa wake wa Twitter, baada ya madai hayo kuibuka hivi karibuni Katika Mitandao ya kijamii.

“Jeshi Polisi limekanusha ujumbe unaosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema hakuna matukio kama hayo, Kibiti ni shwari na salama. Upuuzeni uzushi huu, pia endeleeni kuwapuuza wasioitakia mema nchi yetu,” imesema taarifa yetu.

Miaka kadhaa iliyopita mauaji ya baadhi ya raia, viongozi wa Serikali za mitaa na Polisi yaliibuka katika wilaya za Mkoa wa Pwani, ikiwemo Kibiti.

Vyombo vya ulinzi na usalama, vilifanikiwa kudhibiti mauaji hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!