Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Balozi Dk. Slaa naye adaiwa kukamatwa
Habari za SiasaTangulizi

Balozi Dk. Slaa naye adaiwa kukamatwa

Spread the love

BALOZI na Mwanasiasa maarufu nchini, Dk. Wilbroad Slaa anadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake Mbweni jijiji Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali, akiwamo Askofu Emmaus Mwamakula zinasema, Dk. Slaa amekatwa leo Jumapili mchana ikiwa ni siku moja baada ya kukamatwa kwa Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyagali.

Dk. Slaa ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ni mmoja wa wanasiasa wanaopinga mkataba wa uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.

 

Kukamatwa kwa Dk. Slaa pamoja Mwabukusi  kumekuja siku chache baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.”

Akiandika kupitia mtandao wake wa kijamii, Askofu Mwamakula anasema,

“taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dk . Wilbroad Slaa amekamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwako jijini Dar es Salaam.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online kwa taarifa zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!