Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Polisi washangaa kukamata waliokuwa wakila uroda barabarani wakidhani majambazi
Kimataifa

Polisi washangaa kukamata waliokuwa wakila uroda barabarani wakidhani majambazi

Spread the love

 

NI kama muvi hivi! Ndivyo unavyoweza kutafsiri mkasa uliowakumba polisi wa kituo cha Ruai katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya, baada ya kuchoma mafuta ya gari yao umbali wa kilomita tano kufukuzia gari lililodhaniwa la majambazi kumbe ni vijana wanne waliokuwa wakivunja amri ya sita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkasa huo ulitokea usiku wa kumakia jana tarehe 22 Oktoba, 2021 baada ya mtu mmoja kupiga simu kituo cha polisi na kudai kuna gari limepaki karibu na nyumbani kwake kwa muda mrefu hadi analitilia shaka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), George Kinoti, maofisa watatu wa polisi katika kituo hicho cha Ruai walipokea ripoti kutoka kwa mkazi mmoja kwamba kulikuwa na gari geni ambalo amelitialia shaka.

“Gari hilo lilikuwa limeegeshwa karibu na kwake muda ya saa tisa usiku lakini pia hakufahamu nia waliokuwa kuliegesha pale ndio maana alihofia kwamba huenda walikuwa na nia mbaya,” amesema.

Ameongeza kuwa, polisi walipofika kwenye eneo la tukio waliona watu wanne wakiingia ndani ya gari lile haraka kisha wakaliendesha kwa mwendo wa kasi na kutoweka.

“Kwa kuwa maofisa wetu walikuwa na hamu ya kufahamu kile ambacho washukiwa wale walikuwa wanafanya, walichukua gari lao aina ya Land Cruiser na kuwafuata mbio.

“Baada ya kuwakimbiza washukiwa kwa takriban kilomita tano bila kufanikiwa kuwakamata, maofisa wetu waliamua kupiga magurudumu ya gari lao risasi na kulifanya lipunguze kasi.

“Gari la washukiwa liliposimama baada ya tairi kuisha upepo, polisi waliona watu wanne waliokuwa uchi wa mnyama wakitoka mule ndani ya gario huku wakiwa wameinua mikono hewani kuashiria kuwa walikuwa wanajisalimisha kwa amani,” amesema.

Amesema watu hao wanne hao walikuwa wanaume wawili na wanawake wawili.

Amesema mmoja wa wanawake wale aliwafahamisha polisi kwamba wao sio wezi ila kosa lao lilikuwa kula uroda wakiwa mahali pasipofaa.

Polisi walishangaa kugundua kuwa juhudi zao za kukamata majambazi ziliwapelekea kuharibu sherehe ya wanne ambao walikuwa wameamua kupeleka burudani yao barabarani.

Hata hivyo, DCI aliwataja wanne hao kuwa ni Vianney Kibet, Silvia Kasiva, Esther Karingari na Denzel Njiru ambao walikamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi pamoja na gari walilokuwa wanalituimia kufanyia ufuska huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Raia Pakistan walilia haki siku ya Mshikamano Kashimir

Spread the loveRAIA wa Pakistani waishio nchini Tanzania wameadhimisha siku ya Mshikamano...

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

error: Content is protected !!