VIONGOZI wa mapinduzi nchini Guinea wametangaza baraza lao la kwanza la mawaziri, linalojumuisha Jenerali wa zamani wa kijeshi na watu wengine watatu waliowahi kushikilia nyadhifa muhimu serikalini chini ya utawala wa Rais Alpha Conde. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Taarifa iliyotolewa jana tarehe 22 Oktoba, 2021 imeonesha kuwa jumla ya mawaziri wanne pekee ndio wameteuliwa na kuacha maswali mengine kwa wachambuzi wa siasa ndani ana nje ya nchi hiyo kwamba yamkini kiongozi wa sasa Kanali Mamady Doumbouya amepanga kuunda baraza dogo.
Msemaji wa jeshi la Guinea amesema Ofisa wa zamani wa jeshi, Aboubacar Sidiki Camara ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa mpito.
Camara aliwahi kuhudumu kama kiongozi wa wafanyakazi katika wizara ya ulinzi chini ya utawala wa Rais Conde na baada ya hapo, akahudumu kama balozi wa Guinea nchini Cuba.
Bachir Diallo, msaidizi wa zamani wa Ulinzi aliyekuwa akihudumu nchini Algeria, ameteuliwa Waziri wa Usalama wakati Louhopou Lamah, mkurugenzi wa zamani wa biashara akiteuliwa kuwa Waziri wa mazingira.
Utawala wa kijeshi umewahakikishia wawekezaji, wafadhili pamoja na serikali za kikanda kuwa mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Conde ni hatua ya mara moja tu ya kile ilichokiita kuondoa mafisadi, na kwamba hauna mpango wa kubaki madarakani.
Leave a comment