Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Jiji la Arusha kinara ukuanyaji wa mapato ya ndani
Habari Mchanganyiko

Jiji la Arusha kinara ukuanyaji wa mapato ya ndani

Jiji la Arusha
Spread the love

 

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imeshika nafasi ya kwanza kwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 6.22 sawa na asilimi 106.8 mapato ya ndani huku halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa ya mwisho kwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 7.78 sawa na asilimia 62.1 katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba, 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Beatrice Kimoleta  wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi cha Robo ya kwanza (Julai –Septemba, 2021 katika Kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa kilichofanyika leo tarehe 23 Oktoba, 2021 Jijini Dodoma.

Amesema kwa upande wa Halmashauri za majiji 6 zimekusanya kiasi cha shilingi bilioni 43.32 sawa na asilimia 89.6.

Kimoleta ameyataja Majiji mengine ni Dar-es-salaam iliyokusanya shilingi bilioni 17.77 (102.1), Tanga shilingi bilioni 3.93 sawa na asilimi 98.5, Mwanza bilioni 4.20 sawa na asilimia 94.8 na mbeya shilingi bilioni 3.41 sawa na asilimia 82.2.

Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Beatrice Kimoleta

Ameendelea kufafanua kuwa katika kipindi cha robo ya kwanza Halmashauri za Manispaa tatu zimefanya vizuri katika makusanyo ikilinganishwa na makadirio yao.

Halmashauri hizo ni Halmashauri ya Manispaa Kahama iliyokusanya shilingi bilioni 2,86 sawa na asilimia 137.2, bukoba bilioni 1.04 sawa na asilimia 129.5 na Halmashauri ya Mpanda ambayo imekusanya shilingi milioni 949.33 sawa na asilimia 116.7.

Kimoleta amezitaja Halmashauri za Manispaa ambazo hazijafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ubungo iliyokusanya kiasi cha shilingi bilioni 5.02 sawa na asilimia 72.5, morogoro shilingi bilioni 1.93 sawa na asilimia 67.0 na mtwara ilikusanya kiasi cha shilingi milioni 725.17 sawa na asilimia 58.6.

Kwa upande wa Halmashauri za Miji Halmashauri ya tatu zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ni Halmashauri ya Mji Mbulu iliyokusanya kiasi cha shilingi milioni 450.71 sawa na asilimia 174.7, kibaha TC shilingi bilioni 1.93 sawa na asilimia 171.6 na Tunduma TC shilingi bilioni 2,20 sawa na asilimia 158.3

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!