Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wajinoa kuboresha ushirikiano na waandishi wa habari
Habari Mchanganyiko

Polisi wajinoa kuboresha ushirikiano na waandishi wa habari

Spread the love

KATIKA kuimarisha mahusiano mazuri baina ya vyombo vya habari na Jeshi la Polisi nchini, jeshi hilo limeshaanza elimu ya utayari kwa askari wake katika kuelekea uchaguzi wa Serikali ya Mtaa mwaka kesho na uchaguzi Mkuu 2025  kwa lengo la kuondoa mitafaruku ambayo huwa hutolea kipindi hicho. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Hayo yamebainishwa jana Jumanne na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP Davidi Misime katika mjadala ulioratibiwa na Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari nchi (UTPC), kupitia Mwamvuli wake wa Klabu ya waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam (DCPC).

Mjadala huo ulihudhuriwa pia na Kamanda wa Polisi Kanda maalam ya Dar es Salaam SACP Jumanne  Muliro, Absalom Kibanda

Misime amemesema mahusiano mazuri kati ya yake na vyombo vya habari yataendeleza umoja na amani nchini ikiwemo uhusiano mema na  jamii.

Pia amesema jeshi lipo kwenye mabadiliko ya kifikra na kufanya vyombo hivyo viwili kuwa na ushirikiano wa karibu katika kutimiza majukumu yao kwani uhusiano kati ya jeshi la polisi na vyombo vya habari hauwezi kuepukika kwa kuwa

SACP Misime ameyasema hayo jana tarehe 17  Oktoba 2023 jijini Dar es Salaam wakati akitoa mada kwenye mdahalo kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya jeshi hilo na waandishi wa habari.

“Nchi itaendelea kuwa na amani na utulivu ikiwa kuna mahusiano mazuri kati ya Polisi na vyombo vya habari, waandishi wa habari na Jeshi la Polisi tunatakiwa tuitangaze nchi yetu vizuri kwa kuwa na mahusiano mazuri na kila pande iheshimu kazi za mwenzake”, amesema Misime.

Amesema jeshi la polisi lipo na falsafa ya kutumia Polisi Jamii, kwa lengo la kutambua mchango na kumshirikisha kila mmoja atambue nafasi yake katika Tanzania kuhakikisha nchi yake inadumisha ulinzi, usalama na mahusiano.

“Ili falsafa hiyo iweze kufanyakazi vizuri, ni lazima jeshi hili lishirikine na vyombo vya habari kwakuwa vina mchango mkubwa na mahusiano ya moja kwa moja na jamii kupitia taaluma zao.

Jeshi la polisi linahitaji zaidi vyombo vya habari na limekuwa karibu na vyombo hivyo husa pale linapotokea suala la taharuki ambapo wamekuwa wakifikisha taarifa kwa umma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji  wa Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya amesema mdahalo huo utasaidia kuondoa changamoto katika vyombo hivyo viwili ambavyo nyakati zingine vimekuwa vikisigana katika kutimiza majukumu yao.

“Mahali kokote ambapo kunakuwa na kutoelewana kunakuwa na uwezekano mzuri wa kuelewana na kupata kesho iliyo bora ndani ya nchi yetu”,alisema Simbaya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema waandishi wa habari na polisi wote wanafanya kazi za kijamii hivyo kuna umuhimu wa kushirikiana na kuleta usawa  ambao utasaidia kuleta maelewano mazuri na kufanya nchi kuwa na twasira nzuri kwa nchi zingine.

“Waandishi zingatieni sheria, haki na wajibu ni muhimu sana, mahusianio yanapotea kati ya taasisi hizi mbili polisi na media/waandishi ni kutokana na kutojua haki zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!