April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Palestina walaani mauaji ya wafungwa Israel

Gereza la Ramla

Spread the love

UBALOZI wa Palestina nchini Tanzania umelaani mauaji ya wafungwa katika magereza ya Israel. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na ubalozi huo leo tarehe 26 Novemba 2019, baada ya Raia wa Palestina, Samir Abu Diyak kufariki dunia, kutokana na kukosa huduma ya matibabu akiwa gerezani nchini Israel.

“Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania unalaani vikali mauaji yanayofanywa na mfumo wa magereza wa Isreali dhidi ya wafungwa wa Palestina, uliopelekea leo hii kifo cha mfungwa Samir Abu Diyak ambaye kwa muda mrefu ameumwa ugonjwa wa Saratani ya utumbo huku akinyimwa huduma sahihi ya matibabu,” inaeleza taarifa ya Ubalozi wa Palestina.

Taarifa ya kifo cha Abu Diyak kimetangazwa leo na Tume ya Masuala ya Wafungwa wa Palestina.

“Tume ya Masuala Wafungwa wa Palestina imetangaza kifo hiki cha kusikitisha leo asubuhi Abu Diyak, mwenye umri wa miaka 37, kutoka kijiji cha Silat al-Dahr kaskazini mwa mji wa West Bank, amefariki dunia katika hospitali ya Israeli ya Asaf Harofeh kutokana na kile Tume ilisema ni sera ya uzembe wa makusudi,”inaeleza taarifa ya ubalozi hiyo.

Kufuatia kifo hicho, ubalozi huo umetoa wito kwa jumuiya za kimataifa kuchukua hatua dhidi ya Israel, kwa kukiuka haki za binadamu na sheria za kimataifa.

“Ubalozi unatoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya Israeli inayoendelea kukiuka haki za binadamu na hali kadhalika sheria za kimataifa, kwa sera zao za ubaguzi na unyanyapaaji.

Pia mamlaka na watu husika wa unyama huu kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya jinai ya kimataifa,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa ya Tume ya Masuala ya Wafungwa wa Palestina imeeleza kwamba,  Abu Diyak alikamatwa mnamo Julai 17, 2002 kwa mashtaka ya kupinga sera za kikoloni za Isreali dhidi ya Wapalestina na kuhukumiwa kifungo cha maisha ambacho ametumikia kwa miaka 17 kabla ya kifo chake.

Abu Diyak aligundulika kuwa na saratani ya utumbo mnamo Septemba 2015, na hali yake ilianza kuzorota baada ya makosa ya ki daktari yaliyofanyika wakati wa upasuaji katika hospitali ya Israel iitwayo Soroka.

Katika upasuaji huo, Abu Diyak alikatwa sentimita 83 za utumbo wake mkubwa, na kuhamishwa na kupelekwa katika kliniki ya gereza la Ramla.

error: Content is protected !!