October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Omar al-Bashir aanza kusulubiwa

Omar al-Bashir

Spread the love

ALIYEKUWA Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ameanza kusulubiwa, Jeshi la nchi hiyo limempeleka katika gereza lenye ulinzi mkali la Kobar, lililoko mjini Khatoum nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, al-Bashir aliyeng’olewa madarakani na jeshi, amewekwa katika chumba cha peke yake huku kukiwa na ulinzi mkali, baada ya kukamatwa jana tarehe 16 Aprili 2019.

Familia ya al-Bashir imethibitisha taarifa ya kukamatwa kwake rais huyo aliyeiongoza Sudan kwa miaka 30, ikisema kwmaba alikamatwa akiwa nyumbani kwake.

Kabla ya kukamatwa, al-Bashir aliwekwa kizuizini na jeshi akiwa nyumbani kwake tangu alipopinduliwa tarehe 11 Aprili 2019.

error: Content is protected !!