Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbowe, wenzake; Jina la Akwelina latajwa
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbowe, wenzake; Jina la Akwelina latajwa

Spread the love

JINA la Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwilin, limetajwa kwenye ushahidi unaotolewa katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Aprili 2019. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Jina hilo limetajwa na shahidi wa Jamhuri, Gelard Ngichi kwenye kesi hiyo ya uchocheza na kwamba, siku  hiyo tarehe 16 Februari mwaka 2018, yeye ndiye aliyepanga vikosi vya askari waliokuwa wakihakikisha usalama.

Shahidi huyo (Ngichi) ni ndio shahidi wa kwanza ambapo ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa Kipolisi Kinondoni.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Thomas Simba, Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi amemtambulisha Afande Rich kuwa ndiye shahidi wa kwanza wa Jamhuri kwenye kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018.

Nchimbi ameiambia mahakama kuwa, shahidi huyo aliyejitambulisha ndio Mkuu wa Operesheni kwenye Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.

Afande Ngichi ndiye aliyepanga vikosi vya askari kulinda usalama siku ambayo wafuasi wa Chadema waliandamana, kupinga mawakala wao kutoapishwa kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kinondoni. Ilikuwa tarehe 16 Februari mwaka 2018.

Siku hiyo watuhumiwa walidaiwa kutenda kosa la kuandamana kinyume cha sheria na kusababisha ghasia, vurugu na kifo cha Akwilin.

Kesi hiyo inaunguruma sasa hivi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo, imeanza kusikiliza ushahidi wa shahidi wa kwanza.

Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni pamoja na Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa; Vicent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Bara.

Wengine ni Ester Matiko, Mbunge Tarime Mjini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini.

Licha ya kosa hilo, watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa 13 pamoa na kufanya uchochezi wa uasi wa kuhamasisha chuki.

MwanaHALISI Online upo mahakamani muda huu kufuatilia kila kinachoendelea kwenye kesi hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!