Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ubalozi Palestina waadhimisha ‘Siku ya Mateka wa Kipalestina’ 
Kimataifa

Ubalozi Palestina waadhimisha ‘Siku ya Mateka wa Kipalestina’ 

Spread the love

BALOZI za Palestina duniani kote, leo tarehe 17 Aprili 2019 zinaadhimisha Siku ya Mateka wa Kiapestina wanaoendelea kushikiliwa na Jeshi la Israel kwenye magereza yao.Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Irene Kitankula, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Ubalozi wa Palestina jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa, mpaka sasa jumla ya raia wa Palestina 6,000 wanashikiliwa kwenye magazeti ya Israel.

“Tayari idadi ya mateka na waliokamatwa waliopo katika magereza ya kivamizi ya Israeli mwaka 2019 imefikia 6000, miongoni mwao wapo watoto 230, wanawake 48 (wakiwemo kina mama 21 na wasichana 8 chini ya umri wa kubaleghe).

“Wapo Wabunge 6, watu 500 waliokamatwa bila ya tuhuma, wagonjwa 1800 wakiwemo 700 wanaohitaji uangalizi wa haraka wa kimatibabu na waandishi wa habari 19,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

taarifa hiyo imeeleza kuwa, mateka 48 wamekamatwa zaidi ya miaka 20 liyopita, wengine 25 wakiwa wamekamatwa tangu robo karne iliyopita, 12 wamekamatwa kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.

“Wengine 29 wakiwa miongoni mwa mateka zamani zaidi waliokamatwa kabla ya Mkataba wa Oslo, ambao walipaswa kuachiwa huru katika awamu ya nne mwezi Machi 2014, isipokuwa utawala wa Israeli ulikataa makubaliano hayo na kuwaweka mateka katika magereza yake,” imeeleza taarifa hiyo.

kwenye taarifa hiyo, imefafanua kuwa zaidi ya mateka 214 wameuawa kwenye taasisi za mateka tangu mwaka 1967; Kati yao, mateka 72 wameuawa kwa kuadhibiwa wakiwa mikononi mwa wachunguzi katika vituo vya uchunguzi.

‘Mateka 60 wameuawa kwa sababu ya kutopewa matibabu, sa wameuawa kwa kukandamizwa na kupigwa risasi na wanajeshi wa Israeli, 75 wameuawa ikiwa ni matokeo ya mauaji ya makusudi,” imeeleza taarifa hiyo.

Taasisi inayoshughulikia mambo ya mateka ya kipalestina imeeleza kwamba, historia ya harakati za mateka wa kipalestina, ilianza mwanzoni mwa uvamizi wa Israeli katika ardhi ya Palesttina mwaka 1948.

Na kwamba, uvamizi wa Israeli ulikwenda sambamba na ukamataji Wapalestina kuwa sera, njia na chombo cha kuwakandamiza na kuwadhibiti.

“Sera hii imetumika na Israeli kama njia ya kuwaadhibu Wapalestina kwa pamoja, huku ikikadiriwa idadi ya kesi za ukamataji katika miaka yote ya uvamizi kufikia zaidi ya kesi 1,000,000,” imeeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the loveHali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!